Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, wanaharakati wa Shirika la Uangalizi wa Haki za Binadamu la Syria wameshuhudia maandamano ya jioni katika kijiji cha al-Mazra‘a kilicho pembezoni mwa Homs, yaliyoitishwa kwa ajili ya kulaani mauaji ya kigaidi dhidi ya Sheikh Rasul Shahoud, mwanazuoni wa Kishia mfuasi wa Ahlul-Bayt (as).
Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Uangalizi wa Haki za Binadamu la Syria, Sheikh shahidi alilengwa kwa risasi moja kwa moja wakati alipokuwa akirejea kutoka katika mashamba ya eneo la al-Wa‘ar, na alifariki papo hapo.
Imeelezwa kwamba maandamano haya yaliambatana na tahadhari kubwa ya kiusalama.
Sheikh Shahoud alikuwa miongoni mwa shakhsia maarufu za kidini katika madhehebu ya Kishia na alikuwa mjumbe wa jopo la kielimu la wafuasi wa Ahlul-Bayt (as). Alikuwa anajulikana kwa juhudi zake katika kuiadhimisha na kuitukuza minasaba ya kidini.
Maoni yako