Jumamosi 12 Julai 2025 - 12:58
Mwanaharakati wa kisiasa wa Bahrain akamatwa

Hawza/ Mamlaka za Bahrain zimemkamata kijana mmoja kwa sababu ya kuchapisha maoni ya kuiunga mkono Iran kwenye mtandao wa Instagram, hatua hii imechukuliwa kama sehemu ya sera za kuendeleza ukandamizaji wa uhuru wa kujieleza katika mitandao ya kijamii.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjuma cha  Shirika la Habari la Hawza, Tovuti ya habari ya Muungano wa Vijana wa Mapinduzi ya 14 Februari imetangaza kuwa utawala wa Aal Khalifa, siku ya Jumatano tarehe 9 Julai 2025 (18 Tir 1404), ulimkamata Hussein Farid Al-Jazairi, mkazi wa mji wa Zahra, kwa kuchapisha maudhui ya kuunga mkono misimamo ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran dhidi ya uvamizi wa utawala wa Kizayuni, kupitia jukwaa la Instagram.

Mwanaharakati huyu wa mitandao ya kijamii, baada ya kukamatwa, alipelekwa kwanza katika ofisi ya mwendesha mashtaka, na kisha aliamriwa kuwekwa kizuizini kwa muda wa wiki moja kwa ajili ya kuendeleza uchunguzi, na hivyo kupelekwa jela.

Hatua hii inachukuliwa huku taasisi za haki za binadamu zikiwa tayari zimekosoa mara kadhaa sera ambazo zinakandamiza uhuru wa kujieleza na kutoa maoni, hasa kuhusu misimamo ya kisiasa inayochapishwa kwenye mitandao ya kijamii.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha