Jumamosi 12 Julai 2025 - 00:23
Kukubali mazungumzo na adui ni kutokuamini ahadi za Mwenyezi Mungu

Hawza/ Rais wa Taasisi ya Imam Khomeini (rah) amesema: Kukubali kufanya mazungumzo na adui ni ushahidi wa wazi wa kutokuamini ahadi ya nusura ya Mwenyezi Mungu na kutokujua kwa hakika njama za adui.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Mahmoud Rajabiy leo Alkhamisi mchana, katika mkutano na wafanyakazi, walimu na watafiti wa Taasisi ya Imam Khomeini (rah), amesema kuwa harakati kuu ya Aba Abdillah al-Husayn (as) ni taswira ya mapambano ya milele kati ya haki na batili, yaliyoanza tangu mwanzo wa uumbaji na yataendelea hadi mwisho wa dunia, na yameenea katika nyanja zote za maisha ya mtu binafsi na jamii kwa ujumla.

Rais wa Taasisi ya Elimu na Utafiti ya Imam Khomeini (rah) ameongeza kuwa: Harakati hii tukufu, kama vile aya za Qur’ani Tukufu zinavyobashiria, ina njia ya kuelekea kwenye ushahidi na kujitolea kwa ajili ya dini, na yeyote atakayeacha kuitembea njia hii, ataingia kwenye mitego ya shetani na kupotoka.

Ayatollah Rajabiy, kwa kuashiria visingizio vya mashetani wakubwa, hasa Marekani na utawala wa Kizayuni unaopora haki, amesisitiza: Mtu anaelegeza msimamo mbele ya ushawishi wa kishetani, si kwamba tu anapotea kutoka kwenye njia ya ufanisi na wokovu, bali pia ataharibika katika kutekeleza majukumu ya kijamii; la kusikitisha ni kwamba baadhi ya viongozi wetu bado hawajafahamu kikamilifu maadui wa dhati wa wananchi na mfumo wetu, na wanadhani kuwa inawezekana kufanya nao mazungumzo na kufikia matokeo yanayoridhisha na kuondoa hatari.

Mwanachama wa Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qom, kwa kuwakumbusha maneno ya rais wa Marekani, amesema: Wakati Trump anaposema wazi kuwa ikiwa mtasalimu amri kama Syria na kukubali matakwa yao basi vikwazo vitaondolewa, na baadhi ya viongozi wetu wakaonyesha kuwa wako tayari kwa mazungumzo, basi huu ni ushahidi wa kutokuamini ahadi za Mwenyezi Mungu na kutokujua kwa kweli njama za adui.

Mjumbe wa Baraza Kuu la hawza amesema: Qur’ani Tukufu inatusihi tuwe na subira na ustahimilivu katika njia ya Mwenyezi Mungu na inatuahidi kuwa yeyote atakayesimama imara mbele ya hila za maadui, atashinda. Na ni wajibu wa kila Muislamu kujilinda na ushawishi wa shetani katika maisha ya binafsi na katika uwanja wa kijamii, kuulinda na kuutunza Umma wa Kiislamu.

Ayatollah Rajabiy huku akinukuu aya za Suratul-Fath amesisitiza: Mwenyezi Mungu anazijua njama zote za maadui, na kila walichopanga kwa ajili ya kuangusha mfumo mtukufu wa Jamhuri ya Kiislamu, kwa fadhila na nguvu ya Mwenyezi Mungu, mipango hiyo imeharibika. Na leo hoja imetimia juu ya kila mtu kuwa ajue kwamba Mwenyezi Mungu yuko pamoja na waja wake, na kwamba sisi lazima tusimame imara mbele ya maadui kwa uwezo wote tulio nao.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha