Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, baada ya kutolewa kwa matamko ya kutisha kutoka kwa Rais wa Marekani dhalimu na viongozi wa utawala wa Kizayuni muuaji wa watoto dhidi ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu na marja'iyya ya Kishia, kundi la waumini waliwasilisha istifta' kwa Ayatollah al-Udhma Makarim Shirazi kuhusu wajibu wa Waislamu mbele ya vitisho hivi. Swali kamili na jibu la mtukufu huyo ni kama ifuatavyo:
Swali: Bismihi Ta‘ala
Mtukufu Marja’ wa wafuasi wa Kishia, Ayatollah al-Udhma Makarim Shirazi (mad-dhillu-hu al-‘āli),
Kwa heshima na salamu,
Katika siku hizi za karibuni tumeshuhudia kuwa Rais wa Marekani pamoja na viongozi wa utawala wa Kizayuni wametishia mara kadhaa kumuua Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu pamoja na baadhi ya wanazuoni na marja’ taqlid.
Tunakuomba utuambie ni ipi hukumu ya kuitishia marja'iyya na uongozi wa jamii ya Kiislamu? Na iwapo — Allah aepushe — kitendo hicho kitatokea kwa mikono ya serikali ya Marekani au mtu mwingine yeyote, ni lipi jukumu la Waislamu duniani kote?
Mwenyezi Mungu awahifadhi na awaunge mkono maulamaa wa Rabbani, marja’ taqlid na Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi chini ya kivuli cha fadhila za Hujjat wa Zama (as), na awaepushe Waislamu na shari za makafiri na maadui wa dini ya Allah.
Wassalaamu 'alaykum wa rahmatullah
"Kundi la waumini na Waislamu"
Jibu la Hadhrat, Ayatollah Makarim Shirazi:
Bismillahir Rahmanir Rahim:
Mtu yeyote au utawala wowote unaonuia kuupiga uma wa Kiislamu na mamlaka yake kwa kuutishia uongozi na marja'iyya, au (la samaha Allah) kuuvunjia heshima, basi hukumu yake ni sawa na "muharib". Na aina yoyote ya kushirikiana au kuupa nguvu utawala huo na watu wake, iwe kwa Muislamu mmoja mmoja au serikali za Kiislamu, ni haramu.Ni wajibu kwa Waislamu wote duniani kuwafanya hawa maadui wajutie kauli zao na makosa yao. Na iwapo hilo litasababisha madhara au kupata hasara yoyote kwa waislamu, basi thawabu yao ni kama ya mujahid katika njia ya Mwenyezi Mungu, inshaAllah.
Mwenyezi Mungu aiepushe jamii ya Kiislamu na shari za maadui, na aharakishe kudhihiri kwa Bwana wa zama, Sahib al-Asr wa al-Zaman.
Daima muwe na mafanikio.
Tarehe 8 Tir 1404
Maoni yako