Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza Matembezi yaliyofanyika mwaka huu Jijini Arusha Tanzania yamefana kuliko miaka yote iliyopita, ukizingatia kwamba jiji la Arusha ni miongoni mwa miji ambayo imetekwa na fikra za kihabi nchini tanzania, lakini Ashura ya Imam Husein mwaka huu imelidhihirisha hilo katika sura ya tofauti baada ya kushuhudia umati mkubwa ambao ulitiririka barabarani kwa ajili ya kumuenzi na kumkumbuka Imam huyo.
Baadhi ya masheikh mbali mbali ambao walishiriki katika matembezi hayo
Umati huu unadhihirisha wazi kwamba madhehebu ya Ahlulbayt (as) katika jiji hilo yanaenea kwa kasi tofauti kabisa na miaka ya hivi karibuni, matembezi hayo yaliyofanyika yaliandaliwa na Huseinia ya Imam Ridha (as), Tasisi ya Katamul-Anbiya pamoja na Taasisi ya Ahlylbayt Center.
Sehemu ya waumini wa kike ambao walishiki kikamilifu katika matembezi hayo
Sehemu nyengine ya waumini wakike ambao waliweza kushiriki katika maombolezo hayo
Maoni yako