Jumamosi 12 Julai 2025 - 00:20
Taasis za kimataifa zilaani mauaji ya maulamaa wa Kishia nchini Syria / Wahalifu na waungaji mkono wa jinai hii katika kanda hii wanapaswa kuhojiwa

Hawza/ Mkurugenzi wa hawza Iran amesema kwa kusisitiza: Mimi binafsi naziomba taasisi zote za kimataifa, hasa Umoja wa Mataifa, Baraza la Haki za Binadamu, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu, Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu na Jumuiya ya Maulamaa wa Kiislamu, kulaani mara moja jinai hizi nchini Syria na kuwahoji wahalifu wa moja kwa moja na waungaji mkono wa kimataifa na wa eneo hili wa jinai hiyo.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah A’rafi, Mkurugenzi wa hawza Iran, katika kulaani mauaji ya maulamaa wa Kishia nchini Syria na kutoa wito kwa taasisi za kimataifa kuchukua hatua ya haraka, ametoa taarifa ifuatayo:

Bismillahir Rahmanir Rahim

Kwa masikitiko makubwa na majonzi, kwa mara nyingine tena mikono michafu ya ugaidi wa kitakfiri na mikondo yenye misimamo mikali inayohusishwa na mfumo wa kibeberu na uzayuni wa kimataifa, kwa kutenda jinai nyingine ya kusikitisha, imewaua kishahidi kundi la maulamaa wakubwa na wabobezi wa Kishia nchini Syria; tukio hili la majonzi si tu kwamba ni ukiukwaji wa wazi wa misingi yote ya kibinadamu, haki za binadamu na dini, bali pia ni ishara dhahiri ya kuendelea kwa mradi hatari wa kutumia dini kama kichocheo cha machafuko na mifarakano katika ukanda huu.

Sisi, sambamba na kulaani vikali jinai hii ya kinyama, tunatangaza kwamba ukimya wa jumuiya za kimataifa na mashirika yanayodai kutetea haki za binadamu mbele ya matukio haya ya mara kwa mara ya maangamizi, unazidisha hali ya ghasia, uchochezi wa chuki za kimadhehebu, na ni tishio kwa usalama wa kimataifa.

Mimi binafsi naziomba taasisi zote za kimataifa, hasa Umoja wa Mataifa, Baraza la Haki za Binadamu, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu, Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu na Jumuiya ya Maulamaa wa Kiislamu kuchukua hatua zifuatazo:

1. Kulaani mara moja jinai hizi na kuwahoji wahalifu wa moja kwa moja pamoja na waungaji mkono wao wa ukanda huu na kimataifa;

2. Kuunda jopo huru la uchunguzi wa ukweli, kwa ajili ya kubaini na kuhifadhi ushahidi wa jinai hizi dhidi ya maulamaa wa dini na walio wachache wa kimadhehebu nchini Syria kwa haraka iwezekanavyo;

3. Kutumia uwezo wa sheria za kimataifa, ikiwemo haki za binadamu, sheria za kibinadamu, na misingi ya haki ya kimataifa ya kijinai, ili kuwafikisha mahakamani na kuwaadhibu waamrishaji na watendaji wa jinai hizi.

Maulamaa wa dini ni wabebaji wa elimu, hekima na amani, na kuwadhuru wao ni sawa na kushambulia mizizi ya ustaarabu wa kibinadamu na urithi wa pamoja wa mwanadamu.

Mwisho, huku nikitoa mkono wa pole kwa familia tukufu za mashahidi waliodhulumiwa, kwa taifa na serikali ya Syria, na kwa wapenzi wote wa haki na uadilifu, nasisitiza kuwa hawza za ulimwengu wa Kiislamu, zikiwa bega kwa bega na mataifa ya muqawama katika eneo hili, zitaendelea kusimama imara katika njia ya kutetea haki, kuimarisha umoja wa umma wa Kiislamu, na kukabiliana na ugaidi ulioratibiwa.

وَسَیعلَمُ الَّذینَ ظَلَموا أیَّ مُنقَلَبٍ یَنقَلِبُون
(Surat ash-Shu‘arā’, 227)

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha