Jumanne 15 Julai 2025 - 14:21
Desturi njema nchini Pakistan ikiambatana na Mwezi wa Muharram

Hawza/ Hujjatul-Islam Sayyid Nusrat Abbas Bukhari, katika hafla ya kugawa miche ya miti iliyopewa jina la "Sabil Ashjar" katika siku za Muharram, alieleza kuwa ubunifu huu ni jibu la kishujaa na la kidini kwa changamoto za mabadiliko ya tabianchi, na akasisitiza kuwa upandaji miti ya Ashura sio tu kuwa ni taswira ya utiifu wa kidini, bali pia ni ishara ya uwajibikaji wa kijamii na wasiwasi wa mazingira wa jamii ya leo.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, taasisi ya Imamiyya Pakistan, mwaka huu pia kama ilivyokuwa mwaka uliopita, iliandaa mpango wa ubunifu kwa jina la "Sabil Ashjar" katika siku za Muharram mbele ya Husayniyya Haydariyya iliyoko katika eneo la Gulgasht, mji wa Multan, Pakistan. Hafla hii ilikuwa mahsusi kwa ajili ya kugawa miche ya miti kwa waombolezaji wa Imam Husein (as); hatua ya ishara iliyolenga kiu ya ardhi na haja yake ya kuwa na uoto wa kijani na hewa safi.

Desturi Njema Nchini Pakistan Sambamba na Mwezi wa Muharram

Katika hafla hiyo ambayo ilifanyika baada ya majlisi ya maombolezo ya Imam Husein (as), mamia ya miche ya miti ilisambazwa kwa waombolezaji. Hatua hii ni muungano wa kufufua desturi ya kidini na kuitikia mahitaji ya kimazingira ya jamii ya leo; hasa katika mji kama Multan unaokabiliwa na joto kali na ukame.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha