Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza la kimataifa, Hadhrat Ayatollah Sistani ametoa bayana yenye maneno makali dhidi ya uvamizi wa Wazayuni nchini, na kila aina ya vitisho dhidi ya Kiongozi wa mapinduzi ya kiislamu ya Irani
بسمالله الرحمن الرحيم
Marjaa tukufu ya dini ya Najaf ashraf imekemea mwendelezo wa uvamizi wa Wazayuni kwenye nchi ya Jamhuri ya kiislamu ya Irani, na kila aina ya vitisho na makusudio mabaya dhidi Kiongozi mtukufu wa dini na siasa, na kwa hakika inatoa tahadhari kila aina ya uovu wa aina hii - kwani ni sawa na kudharau misingi ya dini na uvunjifu wa wazi wa kanuni za kimataifa - utaleta tija mbaya katika ukanda huu, tija ambayo itapelekea kutokudhibitika, na kuleta sintofahamu ambayo itasababisha maumivu kwenye mataifa yaliyopo ukanda huu, na manufaa yao yote yatakuwa kwenye hatari.
Kwa sababu hiyo kwa nguvu zetu zote tunaziomba taasisi zote zenye athari kimataifa na dola za ulimwenguni, zijitahidi katika kuvisimamisha vita hivi vya dhulma, na watafute njia salama na ya uadilifu kwa ajili ya faili la nyuklia ya Irani kwa mujibu wa kanuni na vigezo vya kimataifa.
Maoni yako