Alhamisi 19 Juni 2025 - 18:44
Muislamu yeyote mzima na alie huru hakubaliani na vitisho vilivyo tolewa dhidi ya kiongozi wa mapinduzi ya kiislamu

Hawza/ Hadhrat Ayatollah Makarrim Shirazi ameweka wazi kuwa; Kupatikana kiongozi adhimu wa mapinduzi, kwa anuani ya kwamba ni mwenye kuhifadhi nembo ya ushia bali uma wa kiislamu, ni nukta muhimu sana katika akida zetu, na Muislamu yeyote mzima na alie huru hakubaliani na vitisho vilivyo tolewa dhidi yake

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, matini ya ujumbe kamili wa Hadhrat Ayatollah Makarrim Shirazi, kutokana na jinai zinazofanywa na wazayuni pamoja na ujasiri dhidi ya kiongozi wa mapinduzi ni kama ifuatavyo:

بسم الله الرحمن الرحیم

وَقَاتِلُوهُمْ حَتَّیٰ لَا تَکُونَ فِتْنَةٌ

Na piganeni nao mpaka pasiwepo fitna.

Zimepita siku chache tangia utawala dhalimu wa Kizayuni kuvamia nchi yetu azizi ya Irani, na kumwaga damu za wasichana na Watoto wasio na hatia Pamoja na kuvamia vyombo vya Habari, Taifa la Irani kwa moyo mmoja, chini ya bendera moja limesimama huku wakiwa pamoja na kiongozi wao na kutarajia nusra ya Mwenyezimungu, taifa la Irani mpaka kuung’oa mzizi wa Israil mwenye kufanya jinai, litavumilia machungu yote na hata zaidi ya haya, na kama hivyo Qurani ilivyo sema:

إِنْ تَکُونُوا تَأْلَمُونَ فَإِنَّهُمْ یَأْلَمُونَ کَمَا تَأْلَمُونَ وَتَرْجُونَ مِنَ اللَّهِ مَا لَا یَرْجُونَ

Mkiwa mnaumia basi nao wanaumia kama mnavyo umia ninyi, nanyi mnatarajia kwa Mwenyezi Mungu wasiyo yatarajia wao.

Taifa hili lina matumani ya msaada wa Mwenyezimungu, na linasubiria kiaga cha mwisho cha Mwenyezimungu mtukufu.

Lakini utawala huu bandia na batili ambao ni dhaifu kabisa, baada ya kushindwa na jeshi la Irani, kwa kutarajia upate msaada kutoka kwa Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya na wafuasi wao, huku baadhi ya nchi katika ukanda huu zinatafuta njia ya kukimbia kutokana na hali inayo endelea katika ardhi haramu ya Israil, mpaka ikafikia wakati wanatoa vitisho vya kifedhuli kwa kiongozi wa mapinduzi ya kiislamu.

Hapa pana nukta kadhaa ni lazima tuziangazie;

Nukta ya kwanza; Kupatikana kiongozi adhimu wa mapinduzi, kwa anuani ya kwamba ni mwenye kuhifadhi nembo ya ushia bali uma wa kiislamu, ni nukta muhimu sana katika akida zetu, na Muislamu yeyote mzima na alie huru hakubaliani na vitisho vilivyo tolewa dhidi yake, hivyo basi ni wajibu kwa kila Muislamu na mwenye kupenda uhuru, duniani kote kwa hali yeyote ile kumkingia kifua, na kuhakikisha kwa kila yule ambae ataonesha ujasiri dhidi yake, basi afahamu kuwa uma wote ulimwenguni utasimama dhidi yake.

Nukta ya pili; vikosi vya jeshi la Irani, kama vile ambavyo mpaka sasa vimeweza kumshinda adui katika Nyanja zote, ni lazima vizidishe ubunifu na kwa kushtukiza kuendelea kumpiga adui mpaka asiwe tena na fikra pamoja na vitisho kama hivi.

Nukta ya tatu; Hakika kile ambacho tupo nacho kila siku na tutaendelea kuwa nacho, nacho ni Imani thabiti waliyokuwa nayo wananchi, hivyo basi ni lazima kwa watu wote na waumini kwa ujumla katika kipindi hiki kigumu washirikiane kwa Pamoja kwenye kumuomba mwenyezimungu, na kutawasali kwa maasumina, kwani adui wenu vyovyote vile awavyo, bado “msaada wa Mwenyezimungu upo juu yao”

Wassalam aaykum

Qum, Naasir Makaarim

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha