Jumapili 15 Juni 2025 - 21:22
Wadai uongo wa Mahdawiyya

Hawza / Kila Mshia mwenye ufahamu anawajibika kuwakadhibisha wale wanaodai kuwa na uhusiano au uwakilishi maalum (niyaba maaluma) na Imamu, na kufunga njia ya kupenyeza na kujinufaisha kwa watu hawa wanaotafuta fursa na wanaiopenda dunia.

Shirika la Habari la Hawza - Moja ya madhara katika mafundisho ya Mahdawiyya ni kuibuka kwa wadai wa uongo katika harakati hii tukufu. Katika kipindi chote cha ghaiba ya Imamu Mahdi (as), watu fulani kwa uongo wamekuwa wakidai kuwa wana uhusiano maalum na Yeye au kwamba wameteuliwa na Yule Mtukufu kuwa katika daraja ya niyaba maalum.

Imamu wa Zama (as) katika barua yake ya mwisho kwa Naibu wa nne, Ali bin Muhammad Samori, amesema wazi:

«يَا عَلِیَّ بْنَ مُحَمَّدٍ اَلسَّمُرِیَّ أَعْظَمَ اَللَّهُ أَجْرَ إِخْوَانِکَ فِیکَ فَإِنَّکَ مَیِّتٌ مَا بَیْنَکَ وَ بَیْنَ سِتَّةِ أَیَّامٍ فَاجْمَعْ أَمْرَکَ وَ لاَ تُوصِ إِلَی أَحَدٍ یَقُومُ مَقَامَکَ بَعْدَ وَفَاتِکَ فَقَدْ وَقَعَتِ الْغَیْبَةُ اَلثَّانِیَةُ فَلاَ ظُهُورَ إِلاَّ بَعْدَ إِذْنِ اَللَّهِ عَزَّ وَجَلَّ وَذَلِکَ بَعْدَ طُولِ اَلْأَمَدِ وَقَسْوَةِ اَلْقُلُوبِ وَامْتِلاَءِ اَلْأَرْضِ جَوْراً وَسَیَأْتِی شِیعَتِی مَنْ یَدَّعِی اَلْمُشَاهَدَةَ أَلاَ فَمَنِ ادَّعَی اَلْمُشَاهَدَةَ قَبْلَ خُرُوجِ اَلسُّفْیَانِیِّ وَ الصَّیْحَةِ فَهُوَ کَاذِبٌ مُفْتَرٍ.»

Ewe Ali bin Muhammad Samori! Mwenyezi Mungu awalipe thawabu kubwa ndugu zako kwa ajili yako. Kwa hakika wewe utakufa ndani ya siku sita zijazo. Kusanya mambo yako, na usimpe wosia yeyote achukue nafasi yako baada ya kifo chako. Hakika ghaiba ya pili itatokea baada ya kifo chako, na hapatakuwa na kudhihiri ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na hilo litakuwa baada ya muda mrefu, na ugumu wa mioyo, na ardhi kujazwa dhulma. Hivi karibuni watu miongoni mwa Mashia wangu watatokea wakidai mush'ahada. Tambueni kwamba yeyote atakayekuja kabla ya kutoka kwa Sufyani na sauti ya mbinguni na kudai mush'ahada(1), huyo ni mwongo na mwenye kuzua. (Kamaal ad-Din, j. 2, uk. 516)

Kwa kauli hii iliyo wazi, kila Mshia mwenye ufahamu anawajibika kuwakadhibisha wale wanaodai kuwa na uhusiano maalum au niaba maalum, na kufunga njia ya upenyezaji na unyonyaji wa watu hawa wanaotafuta fursa na wanaotaka dunia.

Baadhi ya waongo hawa wamepiga hatua zaidi, na baada ya kudai niaba wameanza kudai wao ndio Mahdi mwenyewe, na kwa dai hili batili wameanzisha madhehebu na makundi ya upotofu na hivyo kuweka mazingira ya upotofu wa kiitikadi kwa watu wengi. Kwa kuchunguza historia ya makundi haya, inadhihirika wazi kwamba mengi yao yameasisiwa na kuendelezwa kwa msaada na uungwaji mkono wa mkoloni.

Ni dhahiri kuwa kuibuka kwa makundi na madhehebu ya upotofu, na kujiunga kwa watu pamoja na kuwaamini wadai wa Mahdawiyya au niyaba, kunachimbuka katika ujinga na kutokuwa na maarifa kwao.

Shauku kubwa ya kumuona Imamu (as) bila ya maarifa na uelewa wa kutosha kumhusu Yeye, pamoja na kughafilika juu ya kuwepo kwa wadanganyifu katika uwanja huu, huandaa mazingira ya kuungana na wadai wa uongo.

Hivyo basi Mashia wanaongoja, wanapaswa kwa maarifa ya kutosha kuhusu mafundisho safi ya Mahdawiyya, kujilinda na mitego ya wadanganyifu, na kwa kufuata maulamaa waaminifu wa Kishia, watembee katika njia iliyo wazi ya madhhabu.

------------------------------------------------------------------
(1) Makusudiwa ya "mushāhada" hapa ni niyaba yenyewe (yaani kudai kuwa yeye ni naibu wa Imamu (as)), si kumuona kwa macho tu.

Utafiti huu unaendelea…

Imenukuliwa kutoka katika kitabu “Negin-e Āfarinish” huku ikifanyiwa marekebisho kiasi

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha