Jumamosi 25 Julai 2026 - 17:16
Haram Tukufu ya Alawi yatangaza mpango wake wa kitabibu, kiafya na huduma zake kwa ajili ya kuwahudumia mazuwari wa Arubaini

Hawza/ Kituo cha Tiba cha "Rasul al-A'dham (saww)" kilicho chini ya Haram Tukufu ya Alawi kimetangaza kukamilisha maandalizi maalumu ya kitabibu na kiafya kwa ajili ya ziara ya Arubaini ya Imam Hussein (as), kupitia utekelezaji wa mpango wa kina. Lengo la mpango huo ni kutoa huduma bora zaidi za matibabu na kuwasaidia mazuwari wanaofika katika Haram Tukufu ya Amirul-Muuminina Imam Ali bin Abi Talib (as).

Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Kituo cha Tiba cha "Rasul al-A'dham (saww)" kilicho chini ya Haram Tukufu ya Alawi kimetangaza kukamilisha maandalizi maalumu ya kitabibu na kiafya kwa ajili ya ziara ya Arubaini ya Imam Hussein (as) kupitia mpango wa kina. Lengo la mpango huo ni kuwapatia mazuwari wanaotembelea Haram Tukufu ya Amirul-Muuminina (as) huduma bora zaidi za matibabu na uokoaji.

Javad Ismaili, Mkuu wa kituo hicho, alisema kuwa; kituo hicho kwa uratibu na idara mbalimbali za Haram Tukufu na kwa ushirikiano na Idara ya Afya ya Najaf Ashraf pamoja na Shirika la Mwezi Mwekundu la Iran, kimefungua vituo vitano vya huduma za kitabibu vinavyoizunguka Haram Tukufu. Vituo hivyo vitakuwa na madaktari, wauguzi, wahudumu wa afya, pamoja na vifaa vya tiba, dawa na mahitaji yote muhimu ya matibabu.

Ismaili aliongeza kuwa; Kituo cha "Qanbar", kinachohudumia wahudumu wa Haram, kitasaidia kuimarisha kikosi cha uokoaji wa dharura kwa kutuma wahudumu wa uokoaji 335, wakiwemo wanaume 210 na wanawake 125. Kikosi hicho kitatoa huduma za uokoaji katika maeneo ya tukio na kuwahamishia wagonjwa wanaohitaji huduma maalumu kwenye vituo vya karibu vya matibabu kwa kutumia magari ya wagonjwa yaliyopo katika maeneo husika.

Haram Tukufu ya Alawi imeweka uwezo wake wote wa huduma, vifaa vya usafirishaji na tiba kwa ajili ya kuhudumia mamilioni ya mazuwari wa Haram Tukufu ya Amirul-Muuminina, Imam Ali bin Abi Talib (as), katika kipindi cha ziara ya Arubaini ya Imam Hussein (as).

Kwa upande mwengine, Mahdi Saleh Mahdi, Naibu Mkuu wa Idara ya Huduma ya Haram Tukufu, alisema kuwa; wafanyakazi wa idara hiyo wameanza kufungua zaidi ya vituo vitano vya kuhifadhi mizigo na mali binafsi za mazuwari. Kila kituo kina uwezo wa kuhifadhi zaidi ya mizigo 2,000, jambo ambalo litasaidia kurahisisha harakati za mazuwari na kuhakikisha usalama wa mali zao.

Aliongeza kuwa; idara hiyo pia imekamilisha uwekaji wa mahema makubwa nane kwa ajili ya malazi ya mazuwari; mahema manne yamewekwa katika Barabara ya Al-Hujjah, na manne mengine katika Mji wa Imam Ridha (as). Kila hema lina ukubwa wa zaidi ya mita za mraba 1,000 na limewekewa mazulia pamoja na vifaa vya kupooza hewa kwa ajili ya kuwahudumia mazuwari.

Aidha, alibainisha kuwa; mpango huo unajumuisha pia kuweka zaidi ya vituo 14 vya kusambaza maji baridi ya kunywa kuzunguka Ukumbi Mtukufu wa Alawi na Mji wa Imam Ridha (as), kufunga zaidi ya vifaa 500 vya kupooza hewa katika eneo la Ukumbi Mtukufu na Ukumbi wa Bibi Fatimah Az-Zahra (as), pamoja na kutandika mazulia katika ghorofa zote tatu za Ukumbi Mtukufu kwa aina mbalimbali za mazulia.

Mahdi aliendelea kueleza kuwa; idara hiyo imepanga kuweka zaidi ya vyoo saba vya muda vinavyohamishika katika njia ya Barabara ya Kufa hadi eneo la Haram Tukufu ya Alawi. Aidha, vyoo vya vilivyopo kuzunguka Ukumbi Mtukufu, katika Mji wa Imam Ridha (as), pamoja na vituo vya huduma vilivyo karibu na nguzo namba 96 na 234, vimekarabatiwa na kuandaliwa kikamilifu ili viwe tayari kuwapokea mazuwari.

Alisisitiza kuwa; sehemu ya maandalizi hayo ilianza zaidi ya mwezi mmoja uliopita, hususan katika ujenzi wa mahema na kuyapamba kwa mazulia pamoja na mifumo ya kupooza hewa.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha