Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, kutokana na mnasaba wa maadhimisho ya mwaka wa thelathini na sita tangia kufariki kwa mwanzilishi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, na kumbukumbu ya mwaka wa sitini na mbili tangia tukio la maasi ya umwagikaji wa damu la tarehe 15 Khordad, Jumuiya ya Walimu imetoa tamko lenye maudhui yafuatayo:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema, Mwingi wa Huruma:
Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yalikuwa ni harakati iliyochimbukia kutoka katika utamaduni wa Karbala, na yakawa ni uteuzi mpya kwa ajili ya kuchomoza tena kwa uislamu. Utukufu wa mapinduzi haya umejikita katika utukufu wa shakhsia ya Imam mtukufu, na mapinduzi haya hayatatambulika kweli pasi na kuwepo jina la Imam Khomeini (ra).
Imam, kwa ujasiri na ukweli wa kauli yake, aliwalingania watu kusimama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na watu kwa kuitikia mwito wa Imam, walimng’oa mtawala wa kidhalimu na wakaamua kuisimamisha serikali ya kimungu. Mabadiliko haya makubwa ndani ya watu yalitokana na baraka ya mafundisho ya uislamu na nguvu ya kumjenga mwanadamu ilikuwa ni sehemu ya Imam.
Umaridadi wa Imam na ushindi mkuu alioupata ilikuwa ni kulea wanaume na wanawake waumini na mujahidina, jambo ambalo linaendelea hadi leo hii. Uislamu halisi wa Muhammadi (saw) kwa ujasiri na jihadi ya wana wa Imam Khomeini mkubwa katika kila pembe ya dunia, unaendelea kukua na kuenea, na mwangaza huu wote umetokana na utukufu wa harakati ya dhati ya Imam Khomeini (ra).
Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qom, kwa kuadhimisha mwaka wa thelathini na sita tangia kutengana na mbeba bendera mkuu wa ujumbe wa kimungu, inaitukuza kumbukumbu ya Imam aliyekuwa na heshima kuu, pamoja na mashahidi wote wa Mapinduzi ya Kiislamu, hasa mashahidi wa tarehe 15 Khordad 1342 (June 5, 1963), na inatangaza kuwa:
Njia ya Imam na fikra zake ni taa ya mwangaza kwa ajili ya kufanikisha malengo yetu ya kimaanawi na kimada. Siasa, uchumi na utamaduni katika fikra za Imam vyote vilikuwa vimechimbuka kutoka kwenye mafundisho ya Ahlul-Bayt (as) na yeye, akiwa ni mfuasi wa kweli wa njia ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alileta tena hazina zilizokuwa zimesahaulika za dini katika uwanja wa maisha, ili kuirudisha hai asili ya umma wa Kiislamu iliyopotea.
Leo hii pia, Kiongozi mwenye busara wa Mapinduzi, Ayatollahil-Udhma Imam Khamenei kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu, subira, ikhlasi na busara, amezishika kwa mikono yake fikra zenye nuru za Imam adhimu na anawalinagania wote kushikamana na malengo ya Imam na Mapinduzi. Mapenzi kwa Imam bila kumtii Kiongozi wa Kidini wa zama hizi, yaani Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ni dai la uongo, na halitakuwa na mwisho isipokuwa upotofu na kuangamia.
Kushikamana na urithi wa Imam – yaani, uongozi wa kidini wa jumla (Wilayatul-Faqih al-Mutlaqa) na kufuata uongozi huo – ndio njia pekee ya kulinda Mapinduzi ya Kiislamu, na Mapinduzi haya, kwa kuzingatiwa na Imam Mahdi (as) yanakaribia kufika kwenye jua la kudhihiri. Kushiriki kwa hamasa katika sherehe za kumbukumbu ya kifo cha Imam mtukufu katika haram yake takatifu, na kufanywa upya kiapo kwa Imam mpenzi Khamenei, kutakuwa ni ushiriki wa kuvunja nguvu za adui, na tunatumaini kwamba wananchi wapendwa kama kawaida yao, watashiriki kwa namna ya kishujaa katika tukio hili tukufu.
Jumuiya ya Walimu wa Hawza (Jamiatul-Mudarrisin) Qom
Maoni yako