Jumatatu 5 Mei 2025 - 09:13
Hawza ya Qum ina mwendelezo wa kimataifa/ Hawza na maulamaa pasi na watu havina maana

Mkurugenzi wa Hawza Irani, katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na wanahabari, alifafanua vipengele vya mabadiliko vilivyo leta athari katika Hawza ya Qum ndani ya kipindi cha miaka mia moja iliyopita.

Kwa mujibu wa  Shirika la Habari la Hawza, kutoka Tehran, Ayatollah A'rafi leo Jumapili, tarehe 4 Mei, katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu kongamano la kimataifa la kumbukumbu ya miaka mia moja ya kuanzishwa upya Hawza ya Qum, alisema: Hawza siku zote imekuwa ikijitokeza kama taasisi inayozingatia elimu na yenye lengo la kutoa huduma, na imekuwa na huduma pana za kimataifa katika sekta za elimu na fikra, mawazo na utamaduni, jamii na watu, na itaendelea hivyo; Hawza itabakia kuwa ni Hawza, iwapo itayahifadhi mambo haya na kuyaenzi.

Mkurugenzi wa Hawza nchini Irani aliongeza kuwa: Misingi ya kielimu ni miongoni mwa vipengele muhimu zaidi vya Hawza, na wasomi wakubwa wamejitokeza ndani ya taasisi hii. Katika zama zilizopita, elimu na maarifa yote yalikuwa yakizalishwa katika Hawza, kwani elimu za kiakili, nakili, na taibia zilikuwa zikifundishwa na kufanyiwa utafiti ndani ya Hawza, lakini baada ya kugawanywa na kufanyiwa utaalamu maalum kwa kila elimu, elimu hizo zilitenganishwa.

Mjumbe wa Baraza Kuu la Hawza alifafanua kuwa: Kipengele cha pili cha Hawza ni pamoja na maadili na hekima ya kimatendo, pamoja na desturi za kale za kiakhlaqi na kiibada katika maeneo mbalimbali. Mabwana wetu katika historia ya zaidi ya miaka elfu moja wameongoza katika uwanja wa hekima ya kielimu, na nyuso mashuhuri zimejitokeza katika Hawza.

Makamu wa Mwenyekiti wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu wa Uongozi (Majlisi Khobregan Rahbari) alisisitiza: Kipengele cha watu na kijamii ni miongoni mwa vipengele muhimu zaidi Hawza. Hawza na uongozi wa kidini havina maana yoyote bila ya watu. Hawza imetokana na watu, na inaandamana na watu. Mafungamano ya kina kati ya wanazuoni wetu wakubwa na watu wa kawaida, na hisia ya kutaka kutoa huduma, ni jambo muhimu sana ambalo limekuwepo na linaendelea kuwepo katika historia ya Hawza. Mwanazuoni wa dini, atakuwa kweli mwanazuoni wa dini, iwapo kwa nafsi yake yote atajiona kuwa mnyenyekevu mbele ya watu na kujiweka kuwa mwenye deni kwa jamii na watu.

Ayatollah A'rafi alikumbusha kwa kusema: Kipengele cha nne cha Hawza kinahusisha siasa sahihi na fikra iliyo sahihi, mbali na misimamo mikali au ya kusuasua katika suala la siasa. Katika uwanja huu, Hawza imekuwa mbeba bendera ya uhuru kwenye mataifa ya Kiislamu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha