Alhamisi 1 Mei 2025 - 07:45
Ayatollahil-‘Udhmaa Nuri Hamadani katika kikao chake na Ayatollah A‘raafi: Katika miaka ya hivi karibuni, mabadiliko makubwa yamejitokeza kwenye Hawza.

Hadhrat Ayatollah Nuri Hamadani katika kikao chake na Mkurugenzi (Mudir) wa Hawza nchini Iran alibainisha kuwa: Bila shaka yoyote, katika miaka hii ya hivi karibuni, shughuli nyingi zimefanyika katika nyanja mbalimbali ndani ya Hawza, na mabadiliko mazuri yamejitokeza.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, Hadhrat Ayatollah Nuri Hamadani katika kikao chake na Ayatollah A‘raafi Mkurugenzi wa Hawza, huku akionesha shukrani kutokana na juhudi zilizofanyika, alieleza kuwa: Bila shaka yoyote, katika miaka hii ya hivi karibuni, shughuli nyingi zimefanyika katika nyanja mbalimbali ndani ya Hawza, na mabadiliko mazuri yamejitokeza.

Mtukufu huyo, aliashiria juu ya Kongamano la kumbukumbu ya marehemu Ayatollahil-‘Udhmaa Haj Sheikh Abdulkarim Haairi Yazdi (rahimahu Allah), na aliongeza kusema: Jambo hili ni la lazima, na inawapasa wanafunzi waheshimiwa waelimike kuhusu athari na vipengele vya shakhsia za wakubwa wetu, na wawachukulie kuwa ni kigezo.

Mujtahid huyu mkubwa, akiashiria kuhusu maadili na kulea wanafunzi kwa marehemu Haj Sheikh Abdulkarim Haairi (rahimahu Allah), alibainisha: Yeye hakuwahi kuweka fedha za wajibu wa kidini karibu naye, bali alikuwa na mtu mwaminifu sokoni ambaye aliziweka kwake kama amana, na yeye mwenyewe mwanzoni mwa mwezi alikuwa akipokea ruzuku kama walivyokuwa wakifanya wengine.
Sifa nyingine yake ilikuwa ni kulea wanafunzi, ambapo wanazuoni wakubwa waliokuwa Qum kama vile Imam Khomeini (Rahmatullahi ‘alayh) na maulama wengine waliokuwa katika miji mingine, kama vile marehemu Mirza Muhammad Thabati, Akhound Hamadani walikuwa na athari kubwa kiasi gani! Hivyo basi, shakhsia hizi lazima zitambuliwe.

Katika mwanzo wa kikao hiki, Ayatollah A‘raafi, Mkurugenzi wa Hawza nchini Irani, aliwasilisha ripoti yake.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha