Kwa mujibu wa ripoti kutoka Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Rostamnejad alielezea masuala ya Qur’ani kuhusiana na maadili pamoja malezi ya binadamu katika kikao cha mwezi mtukufu wa Ramadhani, kilichofanyika katika ofisi ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, iliyofanyika jioni ya Jumanne katika Husseiniya ya Imam Khomeini (r.a) mjini Qum.
Mjumbe wa bodi ya chuo cha Al-Mustafa alianza kwa kuelezea maeneo matatu muhimu ya maadili katika Qur’ani na kusema: Katika Qur’ani kwa uchache kuna sehemu muhimu tatu zinazo husiana na maadili: Sehemu inayo husiana na vitendo pamoja tabia, ambapo sehemu hii ni mwonekano wa nje wa uwepo wa binadamu; Sehemu inayohusiana na nafsi pamoja na batini, sehemu hii inahusiana na sifa batini za binadamu; Na sehemu inayo husiana na fikra pamoja na maarifa. Kila moja ya sehemu hizi ina kanuni mathubuti na ngumu katika Qur’ani kanuni ambazo zinahukumu maisha yetu.
Hujjatul-Islam wal-Muslimin Rostamnejad akisisitiza kuwa; Qur’ani ni kitabu ambacho kinamlea mwananadamu na kuitakasa nafsi, aliongezea kwa kusema: Qur’ani inatumia njia mbalimbali, kama vile kuweka wazi misingi inayoongoza maisha ya binadamu, ili kufundisha na kuijenga tabia ya binadamu, mojawapo ya mbinu hizi ni kuelezea kanuni ambazo pengine wengi wetu hatujui kama zipo.
Akiashiria jukumu kubwa la Mtume Muhammad (s.a.w) katika kufundisha na kutakasa wanadamu, alisema: Kuitakasa nafsi na malezi ya binadamu ndio falsafa kubwa ya kuletwa Mitume. Qur’ani imesisitiza jambo hili mara kadhaa, ikiwa ni pamoja na aya inayosema: (Yeye atawatakasa na kuwafundisha Kitabu na Hikima). Kufundisha ni hatua ya awali ili uweze kuufikia utakaso, na hili linaonyesha umuhimu mkubwa wa kuitakasa nafsi katika dini ya Kiislamu.
Mwalimu wa Hawza ya Qum, aliendelea kwa kuelezea misingi ya Qur’ani inayohukumu vitendo vya binadamu kwa kusema: Qur’ani inatufundisha kuwa kila amali njema au mbaya ina athari ya moja kwa moja kwa binadamu mwenyewe, hata ikiwa unadhani kwamba kwa kutenda wema unawasaidia wengine, ukweli ni kwamba unajisaidia mwenyewe, mtazamo huu wa Qur’ani kuhusu amali unaweza kuwa ni motisha kubwa katika kutenda mambo mema.
Mjumbe wa bodi ya elimu ya chuo cha Al-Mustafa aliashiria umuhimu wa vitendo vya binadamu katika kutengengeneza hatima yake kwa kusema: Vitendo vyetu tunavyo vifanya leo hii si tu kwamba vinautengeneza utu wetu, bali pia ni mustakbal wa amali zetu za kesho.
Qur’ani inatufundisha kwamba hatima ya binadamu ni matokeo ya moja kwa moja ya vitendo vyake alivyo vifanya katika maisha yake yote, Hivyo basi, lazima tuwe makini jinsi tunavyopanga mawe ya ujenzi wa uwepo wetu, kwa sababu mawe haya yatadhihirika Siku ya Qiyama.
Maoni yako