Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, katika siku ya kwanza ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu jioni ya leo "Katika Hafla ya Ukaribu na Qur'an na katika mkusanyiko wa Maprofesa na Wasomaji wa Qur'an Mashuhuri na wa Kimataifa", akiashiria juu ya uwepo wa haja ya mtu binafsi, kijamii na kitaifa kwa mafundisho ya uponyaji ya Qur'an, amesisitiza akisema: Jamii ya Qur’an inapaswa kutenda kwa namna ambayo chemchem ya kiroho ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu inatiririka katika nyoyo, fikra na hatimaye katika tabia na matendo ya watu wote.
Hadhrat Ayatollah Khamenei ambaye alisikiliza visomo vya wasomaji mashuhuri kwa zaidi ya saa mbili na nusu, katika mkusanyiko na Tawashih za makundi ya ndani na nje ya nchi, aliwapongeza Waumini kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kuwa Mwezi huu ni Eid Kuu na ya kweli ya Waumini na akamtukuza na kumhimidi Mola Mlezi kwa ongezeko endelevu la wasomaji wa Qur'an Tukufu hapa nchini, na akasema: Haja ya jamii kwa vyanzo visivyoisha vya Qur'an ili kuponya matatizo mbalimbali ni hitaji kubwa na la kweli (la hakika).
Katika kueleza mahitaji ya mtu binafsi kwenye Kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu, alisema: Tiba ya magonjwa yote ya kiroho na kimaadili ya Wanadamu kama vile husuda, ubakhili, tuhuma, uvivu, ubinafsi, kiburi na kupendelea maslahi ya mtu binafsi badala ya maslahi ya pamoja (jamii), imo ndani ya Qur’an Tukufu.
Kiongozi wa Mapinduzi pia alisema katika uwanja wa mawasiliano ya ndani ya jamii: Katika kutatua matatizo ya kijamii, ikiwa ni pamoja na haki ya kijamii, ambayo ni suala muhimu zaidi la Uislamu baada ya Tauhidi, tunahitaji kuirejea Qur'an.
Hadhrat Ayatollah Khamenei aliisoma Qur'an kama muongozo ulio wazi (bayana) na sahihi katika nyanja ya mawasiliano (na mahusiano) na nchi zingine, na kuongeza: Taifa la Iran halina tatizo na mataifa mengine, lakini leo hii linakabiliwa na sura pana ya makafiri au wanafiki walioko madarakani, ambapo Qur'an Tukufu imebainisha namna ya kukabiliana nao katika hatua tofauti, ni lini tunapaswa kuzungumza nao, katika hatua gani tunapaswa kushirikiana (nao), ni lini tuwapige ngumi mdomoni, na ni lini kuchomoa upanga.
Alizingatia usomaji sahihi na usikilizaji sahihi wa Qur’an ili kuponya magonjwa yote yaliyotajwa, na akaongeza: “Qur’an inaposomwa vyema na kusikilizwa (vizuri) hujenga hamasa ya kheri na wokovu ndani ya nafsi ya mtu.
Akinukuu Aya kutoka ndani ya Qur'an Tukufu, Kiongozi wa Mapinduzi alibainisha kuwa makusudio ya Mtume (s.a.w.w) katika kuzisoma Aya Tukufu za Qur'an, ni kuitakasa nafsi ili kuponya magonjwa yote ya nafsi na roho, ufundishaji wa Kitabu (Qur'an) maana (na makusudio) yake ni kufundisha mfumo wa jumla wa maisha ya mtu binafsi na ya kijamii, na kufundisha hekima kuna maana ya kutoa elimu ili kujua ukweli (uhakika) wa ulimwengu wa uhai, na akaongeza: Kusoma (Qur'an kwa utaratibu) ni kazi ya kiutume, na kwa hakika wasomaji wa Qur'an Tukufu wanafanya kazi ya Mtume.
Amezingatia kugeuza maana (mafahimu) za Qur'an kuwa uhakika wa kifikra wa watu kuwa ni miongoni mwa kazi muhimu za usomaji sahihi na akasema: Wasomaji wanapaswa kusoma kwa namna ambayo maelfu ya anwani na vichwa muhimu vya Qur'an vinabadilishwa katika akili na fikra za watu na kuwa msingi wa vitendo.
Hadhrat Ayatollah Khamenei amesema: Kisomo kizuri kinaongeza elimu ya watu ya Qur'an, na akasema: Kisomo kinafanya miujiza katika nyanja zote, kwa sharti adabu (ya usomaji) ichungwe na kufuatwa.
Kiongozi wa Mapinduzi aliichukulia hisia halisi ya kuwepo mbele ya Mwenyezi Mungu kuwa ndiyo adabu muhimu zaidi ya kusoma Qur'an Tukufu, na akasema: Qur'an inapaswa kusomwa kwa kuzingatia maana na kwa utaratibu ili iwe na matokeo (chanya).
Katika kueleza maana sahihi ya Tartil (kusoma kwa utaratibu) aliongeza: Tartil ni jambo la kiroho na lina maana ya kusoma kwa utaratibu, kwa ufahamu, kwa kutafakari (tadaburi) na kutua. Bila shaka, kinachofanywa nchini kama Tartil ni kizuri na ni chenye thamani na kinapaswa kuwa maarufu zaidi.
Katika mapendekezo mengine, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi amesisitiza kuwa, lengo la msomaji liwe kwanza kabisa kunufaika na kuathiriwa na maneno yenye nuru ya Wahyi, na kisha kuwa na taathira kwa hadhira, na akasema: Ukitilia maanani lengo hili, hakuna tatizo katika kutumia mpangilio mzuri wa sauti na toni, kama vile wasomaji wetu wa leo hii, kwa kutumia toni nzuri, nyingi zikiwa si za kuiga, huunda unyenyekevu na hali ya dhikri na utukufu katika nyoyo za wasikilizaji.
Ameuona ufahamu wa maana (unapokuwa unaisoma Qur'an) kuwa ni muhimu katika ufanisi wa usomaji na akaongeza: Leo, ikilinganishwa na mwanzo wa Mapinduzi, wasomaji wetu wana ujuzi na ufahamu mzuri wa maana (mafahimu) za Maneno (Aya za Qur'an) na Wahyi, lakini ufahamu wa maana za Aya unapaswa kupanuliwa katika ngazi ya jumla, na ni jukumu la Elimu na Malezi, Jumuiya ya Tablighi ya Kiislamu na Taasisi nyinginezo za Qur'an kutafuta njia za kufanya hivyo.
Suala la "Uso na Sura ya Wasomaji" lilikuwa ni suala jengine ambalo Hadhrat Ayatollah Khamenei aliliashiria na kusema: Pamoja na tabia njema, uso wa msomaji (kwa maana muonekano wa msomaji) pia unapaswa kuwa mzuri na kuwa katika hali ya uadilifu na wa kiroho.
Akigusia safari za Wasomaji wa Kiiran katika nchi za nje na mapokezi yao mazuri, ameona kuwa ni fadhila kuvaa nguo za Kiiran katika hafla za Qur'an nje ya nchi na akasema: Suala jingine ni kutotumia lafudhi ya haram katika usomaji (Tartil).
Maoni yako