Kwa mujibu wa kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Harakati ya Tawhidi al-Islami ya Lebanon katika tamko lake ilieleza: “Shambulio la Israel lililolenga uongozi wa Hamas mjini Doha, na kuendelea kwa jinai ya Kizayuni katika kutekeleza mauaji ya halaiki ndani ya Palestina na ulimwenguni kote, si jambo la ajabu au lisilo la kawaida, bali ni mwendelezo wa siasa ya uhalifu ulioandaliwa na ni hatua inayoeleweka kuelekea ugaidi wa kiserikali chini ya uungaji mkono wa kipekee wa Marekani.”
Harakati hii inalaani uvamizi huu mpya na inasisitiza kuwa: “Mabomu na makombora yamepiga moja kwa moja Baraza la Ushirikiano la Ghuba, Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na pia uongozi wa Qatar – hasa ikizingatiwa kwamba Qatar ilikuwa ikijidhihirisha kama mpatanishi mwenye heshima na anayekubalika.”
Harakati ya Tawhidi al-Islami ikaendelea kusema: “Mwitikio unaostahili wa kila nchi duniani mbele ya kitendo kama hiki kilichofanywa na Israel ni kusitisha uhusiano na dola hii ya kinyama, kufunga balozi zake, na kukatiza kila aina ya uratibu wa kiusalama na kiuchumi, nchi zetu pia zinapaswa kuchukua hatua hiyo, na kisha kusitisha usafirishaji wa mafuta ili kuwa chombo cha kuibana jamii ya kimataifa katika kumdhibiti Netanyahu, Trump na genge lote hili, vinginevyo, nchi zetu zote zitageuka kuwa mataifa yanayovunjiwa heshima na kunyang’anywa mamlaka zao.”
Maoni yako