Alhamisi 10 Septemba 2026 - 10:27
TIC Yamuenzi Sheikh Abdallah Seifu: Sheikh Mkuu wa Mashia Tanzania, Aongoza Hauli na Dua Lindi

Hawza/ Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Tanzania (TIC), Maulana Sheikh Hemed Jalala Mwakindenge, jana Jumatano ameongoza zoezi la kisomo cha Khitma na dua maalumu kwa ajili ya kumuombea marehemu Sheikh Abdallah Seifu Linganaweka, aliyekuwa Sheikh Mkuu wa kwanza wa Jumuiya ya Shia Tanzania.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, hafla hiyo ya kumuombea marehemu imefanyika katika Mkoa wa Lindi, Kijiji cha Mnongong'ole, eneo ambalo ndipo alipozikwa marehemu Sheikh Abdallah Seifu. Zoezi hilo lililenga kumuombea marehemu kwa Mwenyezi Mungu amsamehe madhambi yake, amrehemu na ampe nafasi njema katika maisha ya Akhera.

Hafla hiyo iliongozwa na Maulana Sheikh Hemed Jalala Mwakindenge, ambaye alishiriki pamoja na masheikh mbalimbali, waumini na wanakijiji waliofika kutoka maeneo tofauti kwa ajili ya kushiriki katika kisomo hicho na kumuombea marehemu. Ushiriki huo umeonesha heshima na mapenzi makubwa ambayo jamii ya Shia Tanzania inaendelea kuwa nayo kwa viongozi wake waliotangulia mbele ya haki.

Aidha, Sheikh Muhammad Abdu, ambaye ni Kaimu Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Tanzania (TIC), naye alihudhuria hafla hiyo, pamoja na viongozi na waumini wengine. Uwepo wa viongozi hao katika tukio hilo umeifanya siku hiyo kuwa ya kipekee katika kuienzi kumbukumbu ya mwanazuoni huyo aliyetoa mchango wake katika ujenzi na maendeleo ya Jumuiya ya Shia Tanzania.

Marehemu Sheikh Abdallah Seifu Linganaweka anakumbukwa kama mmoja wa viongozi muhimu katika historia ya Jumuiya ya Shia Tanzania, hususan kwa kuwa ndiye aliyekuwa Sheikh Mkuu wa kwanza wa jumuiya hiyo. Khitma na dua hiyo imekuwa pia fursa ya kuendeleza utamaduni wa kuwakumbuka waliotangulia mbele ya haki, kuenzi mchango wao na kuwaombea rehema kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt).

TIC Yamuenzi Sheikh Abdallah Seifu: Sheikh Mkuu Aongoza Hauli na Dua Lindi

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha