Shirika la Habari la Hawza, limechapisha riwaya ifuatayo kutoka katika kitabu Majmū‘atu Warām.
Imam Hasan al-Mujtaba (a.s.) amesema:
أُوصِیکُمْ بِتَقْوَی اللَّهِ وَإِدَامَةِ التَّفَکُّرِ، فَإِنَّ التَّفَکُّرَ أَبُو کُلِّ خَیْرٍ وَأُمُّهُ
Ninawahusia kumcha Mwenyezi Mungu na kuendelea kutafakari; kwani hakika kufikiri ni baba na mama wa kila kheri.
Tanbīhu al-Khawātir wa Nuzhatu al-Nawādhir (Majmū‘atu Warām), Juzuu ya 1, uk. 60.
Funzo tunalolipata kupitia riwaya hii
Riwaya hii inatufundisha kwamba: Thamani ya mwanadamu imo katika hazina ya fikra na kufikiri kwake, miongoni mwa sifa bora kabisa zinazomtenganisha mwanadamu na viumbe vingine katika mfumo wa uwepo, ni kuwa kwake na fikra, akili na uwezo wa kutafakari.
Maoni yako