Jumatano 9 Septemba 2026 - 16:57
Malezi ya Kielimu na Kidini kwa Kizazi cha Vijana ni Jambo Lisiloweza Kupuuzwa

Hawzah/ Hujjatul-Islamu wal-Muslimin Sayyid Sajid Ali Naqavi amesisitiza umuhimu wa malezi ya kielimu na kidini kwa kizazi cha vijana, na kusema: “Ushindani wenye afya ya kielimu baina ya shule za kidini unatoa mazingira ya kukuza na kuibua vipaji vya wanafunzi wa masomo ya dini.”

Kwa mujibu wa kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, mashindano ya 18 ya kila mwaka ya Qur’ani na Hadithi yaliandaliwa na mwakilishi wa Pakistan wa Jamiatul-Mustafa al-Alamiyyah, na hafla ya kufunga mashindano hayo ilifanyika ndani ya Jamiatul-Kauthar, Islamabad, huku ikihudhuriwa na kundi la wanazuoni, viongozi wa Hawzah, walimu pamoja na wanafunzi wa masomo ya dini.

Katika awamu hii ya mashindano, kundi la wanafunzi wa kike na wa kiume pamoja na watafiti kutoka shule na vituo mbalimbali vya kidini katika maeneo tofauti ya Pakistan walishiriki, na kushindana katika taaluma zinazohusiana na Qur’ani Tukufu na elimu za Hadithi.

Katika hafla ya kufunga mashindano hayo, Hujjatul-Islamu wal-Muslimin Sayyid Sajid Ali Naqavi, Mwenyekiti wa Baraza la Wanazuoni wa Kishia Pakistan, huku akipongeza shughuli za kielimu na kidini za mwakilishi wa Pakistan wa Jamiatul-Mustafa al-Alamiyyah, alisisitiza umuhimu wa kupanua programu za kielimu na kiutamaduni, pamoja na kuweka mazingira ya kuwatambua na kuwaendeleza vijana wenye vipaji vya kielimu.

Alisema: “Malezi ya kielimu na kimawazo ya kizazi cha vijana, pamoja na kuimarisha uhusiano wao na elimu na maarifa ya kidini, ni miongoni mwa mahitaji muhimu na ya msingi ya jamii ya leo, na vituo vya kidini pamoja na Hawzah zinapaswa kuwa na nafasi yenye ufanisi zaidi katika uwanja huu.”

Mwenyekiti wa Baraza la Wanazuoni wa Kishia Pakistan pia aliongeza: “Kupanuka kwa mwingiliano wa kielimu baina ya shule na vituo vya kidini, pamoja na kuunda mazingira ya ushindani wenye afya wa kielimu, kunaweza kuwa na nafasi muhimu katika kuwatambua, kuwaimarisha na kuendeleza vipaji vya kielimu na kimawazo vya wanafunzi wa masomo ya dini na watafiti.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha