Jumanne 8 Septemba 2026 - 21:24
Mtawa Mkristo Azungumzia Miaka 30 Aliyoishi na Waislamu

Hawza/ Bwana Madj, baada ya kutumikishwa kwa muda wa miaka 30 na Vatican nchini Turkmenistan, amesema: “Utamaduni wa Uislamu na Ukristo unakaribiana sana, na sasa nimefikia hitimisho kwamba mawasiliano yenye kujenga baina ya dini hayapatikani kupitia tangazo moja au hafla kubwa, bali hutokea kupitia mazungumzo ya kawaida baina ya watu.”

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha Tafsiri cha Shirika la Habari la Hawza, Bwana Madj, ambaye alitumwa na Vatican akiwa mhubiri wa kidini kwenda katika kanisa moja nchini Turkmenistan, baada ya miaka 30 na mwishoni mwa kipindi chake cha utumishi alisema: “Nilijaribu kushiriki katika furaha na huzuni za watu wa huko, wawe Wakristo au Waislamu, na hata nilialikwa kwenye sherehe za harusi na shughuli za mazishi.”

Akisifu tabia ya kimaadili na kijamii ya Waislamu, alisisitiza: “Ninafurahi kushuhudia uwepo wangu miongoni mwa Waislamu. Katika kipindi cha miaka yote hiyo, nilishawishika kwamba kuheshimiana kunawawezesha Wakristo kuishi miongoni mwa Waislamu na kujenga mahusiano yanayozingatia amani.”

“Utamaduni wa Uislamu na Ukristo unakaribiana sana, na sasa nimefikia hitimisho kwamba mawasiliano yenye kujenga baina ya dini hayapatikani kupitia tangazo moja au hafla kubwa, bali hutokea kupitia mazungumzo ya kawaida baina ya watu.”

“Wakristo wa Turkmenistan wameishi kwa amani na urafiki kwa karne nyingi pamoja na Waislamu walio wengi na wenye heshima kwenye nchi hii.”

Chanzo: Shirika la Habari la Vatican.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha