Shirika la Habari la Hawza – Hujjatul-Islamu wal-Muslimina Muhammad Hussein Mukhtari, Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Vatican, katika makala yenye kichwa “Kulenga Heshima ya Kibinadamu”, ameandika:
Katika siku hizi ambazo dunia inashuhudia tena matumizi makubwa ya nguvu za kijeshi katika eneo hili, picha mbili kutoka kusini mwa Iran hazipaswi kufutika katika kumbukumbu ya fikra na mtazamo wa umma wa dunia: picha ya wanafunzi wa kike waliouawa kishahidi katika shambulio la Marekani dhidi ya shule moja mjini Minab, na picha ya familia za mjini Sirik ambazo sherehe zao za harusi ziligeuka kuwa tukio la maombolezo na huzuni.
Mashambulizi haya mawili, licha ya tofauti zao zote za nje, yana jambo moja la msingi linalofanana: wakati uvamizi wa kijeshi unapovuka mipaka ya kibinadamu na kisheria, mwathirika wa kwanza huwa ni heshima ya mwanadamu.
Shambulio la kijeshi la Marekani dhidi ya Iran, kwa mtazamo wa Jamhuri ya Kiislamu, ni uvamizi wa wazi dhidi ya mamlaka na uadilifu wa eneo la nchi huru; ni hatua ambayo haiwezi kuondolewa au kufutwa asili yake ya kisheria na kibinadamu kwa kutumia lugha za kisiasa, simulizi za vyombo vya habari au visingizio vya kijeshi.
Chanzo: Agenzia Stampa Italia
Maoni yako