Jumatano 9 Septemba 2026 - 09:32
Hadithi ya Leo | Athari za Kujitosheleza na Mwenyezi Mungu

Hawzah/ Imam Ali (as), katika riwaya, anaeleza kuhusu athari za mwanadamu aliejitosheleza na Mwenyezi Mungu kwa kumfanya yeye kuwa tegemeo lake pekee.

Shirika la Habari la Hawza, limechapisha riwaya ifuatayo kutoka katika kitabu “Kashful-Ghummah”.

Imam Ali (as) amesema:

«مَنِ اِسْتَغْنَی‌  بِاللَّهِ اِفْتَقَرَ اَلنَّاسُ إِلَيْهِ وَمَنِ اِتَّقَی‌ اَللَّهَ أَحَبَّهُ اَلنَّاسُ وَ إِنْ كَرِهُوا»

“Mwenye kujitosheleza kwa Mwenyezi Mungu, watu watamhitajia yeye; na mwenye kumcha Mwenyezi Mungu, bila shaka atapendwa na watu, hata kama watakuwa si wenye kulifurahia hilo.”

Kashful-Ghummah fi Ma‘rifatil-A’immah, Juzuu ya 2, uk. 347.

Funzo tunalolipata katika hadithi hii

Hadithi hii inatufundisha kwamba utajiri na kujitosheleza kwa kweli si kuwa na mali nyingi, bali ni kumtegemea Mwenyezi Mungu na kutokuwa na utegemezi wa kupindukia kwa viumbe. Mtu anayemtegemea Mwenyezi Mungu kwa moyo wa dhati hupewa heshima na utukufu, kiasi kwamba badala ya yeye kuwahitaji watu, watu ndio humhitajia yeye.

Pia hadithi inatufundisha umuhimu wa uchamungu (taqwa). Mtu anayemcha Mwenyezi Mungu na kujiepusha na mambo anayoyakataza, Mwenyezi Mungu huweka upendo wake katika nyoyo za watu. Hivyo, upendo wa kweli wa watu haupatikani kwa kujipendekeza kwao, bali kwa kujenga uhusiano mzuri na Mwenyezi Mungu na kuwa na tabia njema.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha