Jumatano 9 Septemba 2026 - 15:56
Leo Tunawahitajia Watu Kama Sheikh Ansa'ri Wanaoendana na Mahitaji ya Zama/ Asisitiza Jihadi ya Kielimu Sambamba na Jihadi ya Ulinzi

Hawzah/ Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walimu wa Hawzah ya Qom, huku akisisitiza umuhimu wa kuendelea na jihadi ya kielimu sambamba na jihadi ya ulinzi, amesema: Sheikh Ansari (ra) katika zama zake alijibu masuala yaliyokuwa yakilikabili jamii kwa kutumia mbinu ya kielimu na kiijtihadi, na akaacha nyuma yake athari za kudumu katika elimu za Fiqhi na Usuli. Leo hii pia tunahitaji Masheikh kama yeye ambao, kwa kina kilekile cha kielimu na mbinu ya kiijtihadi, watachunguza masuala ambayo jamii inayahitajis.

Kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Sayyid Hashim Huseini Bushehri, Rais wa Jumuiya ya Walimu wa Hawzah ya Qom, akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa mwaka wa 29 wa masomo wa (Jumuiya ya Kielimu na Utafiti ya Maimamu Watoharifu) ya Qom, huku akiwapongeza kwa kuanza mwaka mpya wa masomo, alisema: “Kwa dhati kabisa nawapongeza na kupelekea salamu za kheri na baraka kutokana na kuanza mwaka wa 29 wa shughuli za taasisi hii yenye thamani, kwa Mkuu wa Jumuiya ya Kielimu na Utafiti ya Maimamu Watoharifu, Mkurugenzi wa jumuiya hii, manaibu wake, wahusika wa shughuli mbalimbali, walimu, wanafunzi wa masomo ya dini na wanazuoni wa taasisi hii.”

Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Wataalamu wa Uongozi, huku akiwakumbuka kwa heshima Imam Khomeini, Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, Mara'ji wakuu wa Taqlidi, wanazuoni wakubwa wa Hawzah, mashahidi wanazuoni wa dini pamoja na mashahidi watetezi wa nchi na mfumo wa Kiislamu, aliongeza: “Kumbukumbu za watu hawa wakubwa na mashahidi hawa zitaendelea kubaki katika historia, na tunapaswa daima kukumbuka jihadi na huduma zao.”

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walimu wa Hawzah ya Qom pia alimkumbuka kwa heshima marehemu Ayatullah al-Udhma Fadhil Lankarani (ra), mwanzilishi wa Kituo cha Fiqhi cha Maimamu Watoharifu, na kusema: “Sina shaka kwamba kufanyika hafla kubwa kama hii, pamoja na kuendelea kwa karibu miongo mitatu kwa shughuli za kituo hiki cha Fiqhi na Jumuiya ya Kielimu na Kiutafiti, kutakuwa jambo la kuufurahisha moyo wa Marjii huyo mkubwa.”

Hairuhusiwi kusimama palepale

Ayatullah Husseini Bushehri, akiendelea na hotuba yake na kurejea riwaya kutoka kwa Imam Musa al-Kadhim (as) kuhusu umuhimu wa mwanadamu kuendelea kusonga mbele na kukua, alisema: “Wanadamu katika maisha yao ya kimwili na kiroho wanaweza kuwa katika hali tatu: kwanza, kusimama palepale na kutopiga hatua; pili, kusonga mbele kuelekea katika ukuaji na ustawi; na tatu, kurudi nyuma na kuelekea katika hali ya kudidimia.”

Aliongeza: “Jambo ambalo limekosolewa katika utamaduni wa Ahlul-Bayt (as) na mafundisho ya Qur’ani Tukufu ni kusimama palepale pamoja na kurudi nyuma; na jambo lililohimizwa ni mwanadamu kusonga kuelekea ukamilifu na utukufu.”

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walimu wa Hawzah ya Qom, akirejea kauli ya Imam al-Kadhim (as) isemayo:

«مَنِ استَوی یَوماهُ فَهُوَ مَغبون»

alisema: “Ikiwa siku mbili za mwanadamu zitakuwa sawa na hakuna mabadiliko yoyote yatakayotokea katika maisha yake, basi mtu huyo amepata hasara.

Mwaka wa kwanza wa mwanafunzi wa masomo ya dini unapaswa kuwa tofauti na mwaka wa pili wa masomo ya dini, na mwaka wa pili nao unapaswa kuwa utangulizi wa ukuaji na maendeleo zaidi katika miaka inayofuata.”

Akieleza kwamba fursa ya maisha haiwezi kurejeshwa wala kufidiwa, alisisitiza: “Ikiwa mwanadamu atapata hasara katika masuala ya mali, huenda akaweza kuirejesha au kuifidia; lakini muda wa maisha uliopotea hauwezi kurejeshwa wala kufidiwa. Ndiyo maana katika riwaya za Ahlul-Bayt (as), mara nyingi imesisitizwa umuhimu wa kuzitumia na kuzithamini fursa.”

Jihadi ya kielimu sambamba na jihadi ya ulinzi haipaswi kusitishwa

Ayatullah Husseini Bushehri, huku akizungumzia hali nyeti ya sasa ya jamii na nchi ya Iran, alisema: “Leo tupo katika mazingira ambayo kivuli cha vita kimetanda juu ya nchi ya Alawiy, Fatimiy na Muhammadiy, na kama ambavyo katika mazingira ya vita uwanja wa jihadi ya ulinzi hausitishwi, vivyo hivyo jihadi ya kielimu haipaswi kusitishwa.”

Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Wataalamu wa Uongozi aliendelea: “Adui akifanikiwa kufikia malengo yake kupitia upenyezaji wa kijeshi na kisiasa, atachukua hatua hiyo. Sambamba na hilo, kuna pia vichocheo vya upenyezaji wa kimawazo na mikondo vinayozusha mashaka, ambavyo ndani ya jamii na katika mazingira ya nje vinalenga misingi ya Uislamu, Ushia, njia ya Fiqhi, Hawzah, Marjaiya na maadili ya juu ya kidini.”

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walimu wa Hawzah ya Qom alisisitiza: “Kwa namna ambavyo wapiganaji katika uwanja wa ulinzi husimama kidete dhidi ya adui na hawamruhusu adui kufikia malengo yake, vivyo hivyo Hawzah zinapaswa kuingia kwa dhati katika uwanja wa kielimu na kimawazo, na kwa kuimarisha msingi wao wa kielimu na kiutafiti, zijibu mashaka na mahitaji ya jamii.”

Aliongeza: “Jihadi ya kielimu, ya ufundishaji na ya utafiti ina umuhimu mkubwa katika mazingira ya leo, na Hawzah haiwezi kubaki bila kujali masuala ya kimawazo, kiutamaduni, kijamii na kielimu yanayoikabili jamii ya leo.”

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walimu wa Hawzah ya Qom aliongeza: “Tukiangalia wanazuoni wa zamani kama Sahib Jawahir, Sheikh Ansari na wanazuoni wengine wakubwa wa Hawzah, licha ya uwepo wa ukomo wa nyenzo na vifaa katika zama zao, waliweza kuacha nyuma yao athari na huduma kubwa za kielimu. Leo pia tunapaswa kujitahidi kuunda taasisi ambazo zinaweza kufuata mfano huo wa kielimu na kimalezi, kwa kuzingatia mazingira na mahitaji ya zama.”

Jumuiya ya Maimamu Watoharifu imeunganisha urithi wa Hawzah na mahitaji ya sasa ya jamii

Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Wataalamu wa Uongozi, akipongeza shughuli za Jumuiya ya Kielimu na Kiutafiti ya Maimamu Watoharifu, alisema: “Kwa mujibu wa taarifa nilizosoma, pamoja na taarifa zilizowasilishwa leo katika hafla hii, kituo hiki kimeweza kuweka uhusiano kati ya Hawzah ya kimapokeo na yale ambayo jamii na mfumo wa Kiislamu unayahitaji leo.”

Ayatullah Husseini Bushehri, huku akizungumzia kuongezeka majukumu ya wanazuoni wa dini baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, alisema: “Tangu siku ambayo Mapinduzi ya Kiislamu yalipopata ushindi, mzigo wa majukumu ya wanazuoni wa dini umeongezeka, na Hawzah inapaswa kuwa na maandalizi makubwa zaidi ya kujibu mahitaji mapya ya jamii na mfumo wa Kiislamu.”

Aliongeza: “Katika kuchunguza shughuli za kituo hiki, inaonekana kwamba sambamba na Fiqhi, Usuli na Tafsiri, pia kumekuwa na uangalizi wa masuala yanayoikabili jamii na mahitaji mapya ya jamii, na vikao mbalimbali vya kielimu vimefanyika kuhusu masuala ya sasa.”

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walimu wa Hawzah ya Qom, huku akieleza kwamba hana taarifa sahihi kuhusu shughuli za vituo vyote vya kielimu, alisema: “Kuhusu kituo hiki, kwa kuzingatia taarifa na ripoti nilizonazo, ninaweza kusema kwamba shughuli zinazoweza kuelezwa zimefanyika katika nyanja mbalimbali za kielimu.”

Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Wataalamu wa Uongozi, pia alimshukuru Ayatullah Jawad Fadhil Lankarani, Mkuu wa Jumuiya ya Kielimu na Kiutafiti ya Maimamu Watoharifu, pamoja na uongozi na timu ya kielimu ya kituo hiki, na kusema: “Huduma zilizofanyika baada ya kufariki dunia marehemu Ayatullah al-Udhma Fadhil Lankarani (ra), kwa hakika ni hatua zenye thamani na za kudumu.”

Kutoa mafunzo kwa walimu na watafiti katika nyanja za kitaalamu

Ayatullah Husseini Bushehri, akizungumzia upana wa shughuli za kielimu za Jumuiya ya Kielimu na Kiutafiti ya Maimamu Watoharifu, alisema: “Uwepo wa walimu wengi katika nyanja mbalimbali za Fiqhi, Tafsiri, masuala mapya ya kifiqhi na nyanja nyingine za kitaalamu, pamoja na kuwaandaa wanafunzi wa masomo ya dini na wanazuoni wenye uwezo, ni dalili ya bidii, juhudi na shughuli za kielimu za taasisi hii.”

Aliashiria miongoni mwa nguvu za kituo hiki kuwa ni kuwa na watu wenye uwezo na wanaoshirikiana kwa moyo mmoja, na kusema: “Miongoni mwa mafanikio ya uongozi wa taasisi hii ni kuwavutia na kushirikiana na walimu pamoja na watu wenye uwezo; kwa sababu kuwa na washirika wanaoshirikiana kwa moyo mmoja, wenye bidii, wanaotakia mema, wanaoifahamu Hawzah na wenye mtazamo wa mbele, ni neema kubwa kwa taasisi ya kielimu.”

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walimu wa Hawzah ya Qom, huku akizungumzia baadhi ya shughuli za kielimu za kituo hiki katika eneo la masuala mapya, alisisitiza: “Kuandaa vikao vya kielimu kuhusu mada kama vile masuala mapya ya kifiqhi, masuala ya kitabibu na mada zinazohitajika na mfumo wa Kiislamu, ni miongoni mwa hatua zinazopaswa kupewa umuhimu.”

Leo tunahitaji Watu Kama Sheikh Ansari wanaoendana na mahitaji ya zama

Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Wataalamu wa Uongozi, akizungumzia nafasi ya kielimu ya Sheikh Ansari, alisema: “Sheikh Ansari (ra) katika zama zake alijibu masuala yaliyokuwa yakiikabili jamii kwa kutumia mbinu ya kielimu na ijtihadi, na akaacha nyuma yake athari za kudumu katika Fiqhi na Usuli. Leo pia tunahitaji watu kama yeye ambao, kwa kina kilekile cha kielimu na mbinu ya ijtihadi, watachunguza masuala ambayo jamii inayahitajia.”

Ayatullah Husseini Bushehri alisisitiza: “Leo hii kuna masuala mapya yanayojitokeza katika nyanja mbalimbali za kijamii, kiuchumi, kitabibu, kielimu na kiutawala, ambayo yanapaswa kuchunguzwa kwa kutumia mbinu sahihi ya kiijtihadi na ndani ya mfumo wa misingi ya Fiqhi na Usuli.”

Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Wataalamu wa Uongozi aliongeza: “Tunapaswa, sambamba na kunufaika na mbinu ya kutoa hukumu za kisheria iliyotumiwa na wanazuoni wa zamani, kuelekea katika masuala mapya na kuzalisha vitabu, risala, makala na athari za kielimu kwa ajili yake.”

Hawzah isije ikanaswa na usasa wa kupindukia

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walimu wa Hawzah ya Qom, huku akisisitiza umuhimu wa kuhifadhi utambulisho wa kielimu na wa Hawzah, alisema: “Hapa ni Hawzah, ni nyumba ya Imam wa Zama (aj) na taasisi ya Imam wa Zama (aj); kwa hiyo hatupaswi kunaswa na usasa wa kupindukia.”

Aliendelea: “Ikiwa mwanadamu atataka kuwasilisha kila jambo kwa sababu tu wengine wanalipenda, na akaondoa ridhaa ya Mwenyezi Mungu, Uislamu, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) na Ahlul-Bayt (as) katika vigezo vyake, hatafikia anakoelekea.”

Ayatullah Husseini Bushehri alisema: “Hawzah inapaswa kubaki imara juu ya misingi yake, na sambamba na kuhifadhi mbinu ya kiijtihadi ya wanazuoni wa zamani, kwa kutumia mbinu hiyo hiyo ya kielimu inapaswa kuelekea katika masuala na matukio mapya ya kijamii na kutoa majibu muhimu ya kielimu na kiijtihadi.”

Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Wataalamu wa Uongozi, huku akizungumzia ushiriki wake katika maonesho ya athari za kielimu za taasisi hii, alisema: “Mimi wakati mwingine nimeshiriki katika maonesho ya athari za kielimu ya kituo hiki, na kwa hakika nimefurahia shughuli zilizofanyika. Jambo linapofanywa kwa ustahiki, linapaswa kusifiwa na kuthaminiwa.”

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walimu wa Hawzah ya Qom, huku akiipongeza Jumuiya ya Kielimu na Kiutafiti ya Maimamu Watoharifu kwa kuanza mwaka mpya wa masomo, alitoa pongezi kwa juhudi za kielimu za walimu, viongozi, wanafunzi wa masomo ya dini na wanazuoni wa taasisi hii.

Zithaminini fursa za kielimu

Ayatullah Husseini Bushehri, huku akizungumzia umuhimu wa kutumia fursa ya kipindi cha masomo, alisema: “Wanafunzi wa masomo ya dini na wanazuoni wanapaswa kuzithamini fursa zao za kielimu na kutumia uwezo wote uliopo ili kuimarisha msingi wao wa kielimu.”

Akisimulia tukio kutoka katika kipindi cha masomo cha Allamah Tabatabai (ra) huko Najaf al-Ashraf, alisema: “Wakati Allamah alipokuwa akisoma huko Najaf, mwalimu wake, baada ya kuona kipawa chake katika falsafa, alimshauri kwamba ili kuimarisha msingi wake wa kielimu, ajifunze pia hisabati.

Allamah, licha ya matatizo mengi, alitafuta mwalimu wa hisabati na katika joto kali sana la Najaf, wakati kati ya swala ya adhuhuri na muda wa kurejea, alikuwa akienda kwenye darasa la mwalimu wake ili kutumia fursa hii kwa ajili ya kuimarisha msingi wake wa kielimu.”

Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Wataalamu wa Uongozi alisisitiza: “Mifano hii inatukumbusha kwamba fursa za kielimu hupita kwa haraka, na wanafunzi wa masomo ya dini wanapaswa kuthamini kipindi chao cha masomo na kunufaika na uwezo wa walimu, vituo vya kielimu na nyenzo zilizopo kwa ajili ya ukuaji wao wa kielimu na kiroho.”

Kwa upande mwengine Ayatullah Husseini Bushehri, akizungumzia uungaji mkono wa Marajii wakuu wa Taqlidi na Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi kuiunga Hawzah, alisema: “Nina hakika kwamba iwapo viongozi wa taasisi hii wangekuwa na uwezo wa kuweka vifaa na nyenzo zaidi kwa ajili ya wanafunzi wa masomo ya dini, wangefanya hivyo kwa kiwango cha uwezo wao; lakini tunapaswa pia kujitahidi kwa kutumia uwezo tulionao na kumuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu aziteremshe kheri na baraka Zake juu ya taasisi hii.”

Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Wataalamu wa Uongozi, mwishoni aliongeza: “Leo Mara'jii wakuu wa Taqlidi na Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi wanaziangalia Hawzah, na hawaruhusu Hawzah ibaki katika matatizo; kwa sababu Hawzah ina mwenyewe, na mwenyewe mkuu ni Imam wa Zama, Hadhrat Baqiyyatullah al-A’dham (aj).”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha