Kwa mujibu wa Idara ya tarjuma ya Shirika la Habari la Hawza, wanazuoni wa Bahrain katika taarifa yao wamesisitiza: Kuhuisha alama na za Sayyid al-Shuhadaa, Abu Abdillah al-Hussein (as), Ahlu al-Bayt wake na Maswahaba wake wenye nyoyo safi, ni heshima isiyotenganishwa na uchamungu na nyoyo safu, na ni shule hai na mpya ambayo katika kila msimu hujenga upya uelewa na mshikamano.
Wanazuoni wa Bahrain wamesema: “Baada ya kumalizika msimu wa maombolezo ya msiba uliompata Mtume Mtukufu (saww) na yale yaliyowapata kizazi chake kitakatifu katika kipindi cha miezi miwili ya Muharram na Safar, na baada ya kunufaika na mafunzo ya kujitolea na kujitoa muhanga katika njia ya dini na itikadi, kuimarisha nguzo za Wilaya kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mmoja asiye na mshirika, pamoja na kuwapenda mawalii wa Mwenyezi Mungu na kujitenga na maadui na madhalimu wao, wa zamani na wa sasa; leo tunasimama kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa mafanikio aliyowajaalia wananchi wa Bahrain wenye imani katika kutoa, kuwa na subira na kusimama imara katika kuhuisha msimu huu wa kiungu ndani ya mwaka huu wa kipekee uliojaa changamoto na matatizo.”
“Ni mwaka ambao wananchi wameumaliza kwa fahari, kwa baraka ya roho yao ya Kihusseini yenye kujitolea; roho ambayo imevunja juhudi zote za kupunguza thamani na kufanya dharau, na imefanya mipango ya kuondoa maudhui ya kidini katika msimu huu na alama za kidini ishindwe, mipango iliyolenga kupora maudhui yao ya kidini ambayo ndio utambulisho wa taifa hili na nchi hii ya kale katika kushikamana kwake na dini, uhusiano wake na dini na utambulisho wake halisi wa Kiislamu wa Kimuhammadi.”
Wanazuoni wa Bahrain wamewashukuru watu wote waliochangia kufanikisha msimu huu mkubwa; wakiwemo wasimamizi wa Husainiya na kamati za maombolezo, mawaidha na makhatibu, wasomaji wa mashairi na wahudumu, kamati zilizosimamia maandalizi, pamoja na vijana wenye imani ambao walitoa juhudi na muda wao. Pia wamewashukuru wanawake ambao walitoa msaada katika sehemu zote za shughuli hizi.
Wanazuoni wa Bahrain wamewataka watu wote kunufaika na mafunzo haya ambayo hayamaliziki pamoja na kumalizika kwa misimu, bali yanapaswa kuwa taa ya kuongoza mwenendo wa kila siku, kusimama imara juu ya misingi na kushikamana na mstari wa Wilaya katika mambo yote ya maisha, ili Imam Hussein (as) aendelee kuwa hai katika mwenendo na namna ya maisha, na si katika kumbukumbu pekee.
Aidha, wamemuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu awape faraja watu wote wanaodhulumiwa na wanaokabiliwa na matatizo, na awajaalie faraja na ukombozi wanyonge popote walipo.
Maoni yako