Jumamosi 4 Julai 2026 - 21:20
Makubaliano ya “Washington” ni Kinyume cha Sheria na Yanapingana na Maslahi ya Kitaifa ya Lebanon

Hawza/ Jumuiya ya "Qawluna wal-'Amal" ya Lebanon imesisitiza kupinga mazungumzo ya moja kwa moja na adui Mzayuni wa Israel, na kutoa taarifa iliyosomwa na Mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Sheikh Ahmad al-Qattan.

Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Jumuiya ya "Qawluna wal-'Amal" ya Lebanon imesisitiza kupinga mazungumzo ya moja kwa moja na adui Mzayuni wa Israel na kutoa taarifa iliyosomwa na Mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Sheikh Ahmad al-Qattan.

Katika taarifa hiyo alisema: "Kwa kuzingatia maendeleo yanayoendelea na yenye kuamua mustakabali wa nchi yetu, na kwa kutegemea wajibu wa kitaifa na wa Kisheria unaotulazimisha kusema ukweli, tunatangaza kwa umma wa Lebanon na vyombo vya habari msimamo wetu wa wazi na wa dhati wa kupinga mwenendo wa sasa kupitia hoja zifuatazo:

Kwanza: Tunapinga kwa ukamilifu na kwa uthabiti kile kinachoitwa 'Makubaliano ya Mfumo wa Pande Tatu' kati ya Lebanon kwa upande mmoja na adui Israel pamoja na adui Marekani kwa upande mwingine, na tunayaona kuwa ni njia isiyowakilisha matarajio ya wananchi wa Lebanon.

Pili: Tunasema wazi kwamba; makubaliano haya hayalengi kabisa maslahi ya Lebanon na wananchi wake, bali ni mwitikio wa shinikizo linalodhoofisha mamlaka ya taifa.

Tatu: Tunaitaka mamlaka ya kisiasa ya Lebanon kurejea mara moja kutoka katika hatua hii na kuyaondoa makubaliano haya ya mfumo, kwa kuzingatia kanuni ya kitaifa na ya kimaadili isemayo: 'Kurejea kutoka katika kosa ni fadhila.'

Nne: Tunasema wazi kwamba; makubaliano haya hayana athari yoyote ya kivitendo kwa Walebanon walio wengi, kwa sababu idadi kubwa ya wananchi wa Lebanon wanayakataa makubaliano ya aina hii na wanashikamana na heshima yao."

Jumuiya hiyo pia ilitaka kwamba: Msimamo na ombi rasmi la mamlaka ya Lebanon liwe ni kuzingatia tu kuondolewa kikamilifu kwa adui Mzayuni wa Israel kutoka katika ardhi ya Lebanon na kurejeshwa kikamilifu kwa maeneo yote ya Lebanon ndani ya mipaka yake ya kihistoria, bila kupunguzwa hata sehemu ndogo.

Taarifa hiyo pia ilisisitiza umuhimu wa kuzuia aina yoyote ya uchokozi dhidi ya Lebanon, na ikaongeza kwamba mazungumzo na adui hayapaswi kufanyika isipokuwa kwa njia isiyo ya moja kwa moja pekee, kwa sababu aina yoyote ya kuanzisha uhusiano wa moja kwa moja na utawala huo vamizi na ghasibu haikubaliki.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha