Jumamosi 4 Julai 2026 - 17:20
Hizbullah Yatoa Wito wa Kushiriki Mikusanyiko ya Wananchi Sambamba na Hafla ya Mazishi ya Imam Khamenei

Hawza/ Kwa mnasaba wa shahada ya Imam wa Wanyonge, Imam Shahidi Sayyid Ali Husseini Khamenei, Hizbullah imetoa wito wa kushiriki katika mikusanyiko ya wananchi nchini Lebanon na katika ngazi ya kimataifa.

Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, kwa mnasaba wa shahada ya Imam wa Wanyonge, Ayatullah Mkuu, Imam Shahidi Sayyid Ali Husseini Khamenei (Quddisa Sirruh), Hizbullah inawaalika wananchi kushiriki katika mikusanyiko ya wananchi nchini Lebanon na katika ngazi ya kimataifa, sambamba na hafla kubwa ya mazishi, itakayofanyika siku ya Jumatano, tarehe 8 Julai 2026 (17 Tir 1405), saa 3:00 usiku, katika Uwanja wa Ashura, Dhahiya  Kusini mwa Beirut.

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu

﴿الَّذِینَ یُبَلِّغُونَ رِسَالَاتِ اللَّهِ وَیَخْشَوْنَهُ وَلَا یَخْشَوْنَ أَحَدًا إِلَّا اللَّهَ ۗ وَکَفَیٰ بِاللهِ حَسِیبًا﴾

"Wale wanaofikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu, wanamuogopa Yeye, wala hawamuogopi yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Mhesabu."

Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema kweli.

Kwa mnasaba wa shahada ya Imam wa Wanyonge, Ayatullah Mkuu, Imam Shahidi Sayyid Ali Husseini Khamenei (Quddisa Sirruh), tunawaalika mshiriki katika mikusanyiko ya wananchi nchini Lebanon na katika ngazi ya kimataifa, sambamba na hafla kubwa ya mazishi yake.

Muda: Jumatano, tarehe 8 Julai 2026 (17 Tir 1405), saa 3:00 usiku.

Mahali: Beirut, Uwanja wa Ashura, Dhahiya ya Kusini.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha