Jumamosi 4 Julai 2026 - 19:20
Shirika la Habari la Anadolu Laripoti Hafla Rasmi ya Mazishi ya Kiongozi wa Zamani wa Mapinduzi ya Kiislamu

Hawza/ Shirika la Habari la Anadolu limechapisha ripoti kuhusu hafla rasmi ya mazishi na kumbukumbu ya Kiongozi wa zamani wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah, Imam Shahidi Sayyid Ali Khamenei, inayofanyika mjini Tehran, na kuripoti kuwa ujumbe wa ngazi za juu kutoka takriban nchi 100 duniani ulihudhuria hafla hiyo.

Kwa mujibu wa Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, kikinukuu Shirika la Habari la Anadolu, hafla rasmi ya mazishi na kumbukumbu ya Kiongozi wa zamani wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah, Imam Shahidi Sayyid Ali Khamenei, inayofanyika katika Mswala wa Imam Khomeini (ra) mjini Tehran kwa kuhudhuriwa na viongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, viongozi wa kisiasa na wa kidini pamoja na ujumbe mbalimbali kutoka nje ya nchi.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, hafla hiyo ilianza kwa kusomwa kwa aya za Qur'ani Tukufu na kutoa heshima kwa mwili wa Kiongozi wa zamani wa Mapinduzi ya Kiislamu, huku shughuli mbalimbali zinazohusiana na hafla hiyo zikiendelea siku nzima.

Anadolu pia iliripoti kwamba ujumbe kutoka takriban nchi 100 duniani ulihudhuria hafla hiyo, ukiwajumuisha wakuu wa nchi wabunge, mawaziri wa mambo ya nje pamoja na wawakilishi maalumu wa serikali mbalimbali.

Shirika hilo la habari, likimnukuu Ayatullah Ahmad Khatami, liliandika kuwa alisema pembeni mwa hafla hiyo:

"Bila shaka shahada hii imeifanya azma yetu kuwa imara zaidi. Maadui wa taifa la Iran, yaani Marekani na Israel, wanapaswa kujua kwamba tutalipiza kisasi kwa damu ya Imam Shahidi wetu na ya mashahidi wote."

Anadolu pia ilikumbusha kuwa Ayatullah Sayyid Ali Khamenei aliuawa kkshahidi katika shambulio la Marekani na utawala wa Kizayuni lililoanza tarehe 9 Esfand 1404 (28 Februari 2026), na kwamba baada ya takriban wiki moja ya shughuli za maombolezo na mazishi, mwili wake unatarajiwa kuzikwa katika mji mtukufu wa Mashhad tarehe 18 Tir 1405 (9 Julai 2026).

Ripoti hiyo iliongeza kuwa ujumbe wa Jamhuri ya Uturuki ulioongozwa na Cevdet Yılmaz, Makamu wa Rais wa nchi hiyo, ulihudhuria hafla hiyo. Pia ujumbe huo uliandamana na Kayhan Türkmenoğlu, Mwenyekiti wa Kikundi cha Urafiki wa Kibunge kati ya Iran na Uturuki, Hasan Turan, mjumbe wa uongozi wa Bunge la Uturuki, Musa Kulaklıkaya, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, pamoja na Hijabi Kırlangıç, Balozi wa Uturuki nchini Iran.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha