Ijumaa 26 Juni 2026 - 09:20
Vikao vya Maombolezo ya Imam Hussein (as) na Matembezi ya Amani Vyafanyika Mjini Moshi, Tanzania + Picha

Hawza/ Waumini wa dhehebu la Shia mjini Moshi, Tanzania, wamefanya vikao vya maombolezo ya Imam Hussein (as) sambamba na matembezi ya amani katika kuhuisha kumbukumbu ya shahada ya mjukuu wa Mtume Muhammad (saww) katika mwezi mtukufu wa Muharram.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Matukio hayo yalifanyika jana, tarehe 25 Juni 2026, ambapo matembezi ya amani yaliandaliwa na JAMAT Khoja na kuhusisha ushiriki wa waumini wengi waliotembea kwa utulivu na nidhamu wakibeba ujumbe wa amani, haki na kupinga dhuluma.

Mbali na matembezi hayo, waumini walishiriki pia katika vikao vya maombolezo (Majlis) vilivyoangazia malengo ya harakati za Imam Hussein (as), mafunzo ya tukio la Karbala, na umuhimu wa kuendeleza maadili ya uadilifu, kujitolea na kusimama dhidi ya dhuluma.

Vikao vya Maombolezo ya Imam Hussein (as) na Matembezi ya Amani Vyafanyika Mjini Moshi, Tanzania + Picha Vikao vya Maombolezo ya Imam Hussein (as) na Matembezi ya Amani Vyafanyika Mjini Moshi, Tanzania + Picha Vikao vya Maombolezo ya Imam Hussein (as) na Matembezi ya Amani Vyafanyika Mjini Moshi, Tanzania + Picha

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha