Jumamosi 20 Juni 2026 - 08:00
Wanazuoni wa Bahrain Watoa Tahadhari kwa Watawala wa Nchi Hiyo: Msizuie Maombolezo ya Muharram

Hawza/ Wanazuoni wa Bahrain wameonya kuhusu matokeo ya kuendeleza sera ya kulenga na kuweka vikwazo dhidi ya jamii ya Mashia.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Wanazuoni wa Bahrain wameonya kuhusu athari za kuendeleza sera ya kulenga na kuwekea vikwazo madhehebu ya Kishia, na kusisitiza kwamba; kuwazuia baadhi ya makhatibu na waombolezaji (maddah) kutekeleza majukumu yao ya kidini katika kuhuisha alama za Husseini ni ukiukaji wa wazi wa uhuru wa kidini.

Wanazuoni wa Bahrain katika taarifa yao wamesema: “Serikali ya Bahrain, katika hatua ya kidhalimu na yenye kuchochea hisia kwa kiwango kikubwa, sambamba na kuanza kwa msimu wa Ashura na mwezi mtukufu wa Muharram, imewazuia baadhi ya makhatibu wa mimbari za Husseini na waimbaji wa nyimbo za maombolezo katika misafara ya waombolezaji kutekeleza wajibu wao wa kidini wa kuhuisha shairi za Husseini.

Hatua hii ni uvamizi wa wazi dhidi ya uhuru wa kidini, ukiukaji wa moja kwa moja wa Katiba ya nchi, na unyakuzi wa haki ya Waumini kutekeleza itikadi zao kwa mujibu wa hukumu za kifiqhi zilizowekwa na Marjaiyya yao ya kidini; mwenendo ambao Bahrain imeufuata kwa mamia ya miaka.”

Wanazuoni hao walisisitiza kuwa; sera hii ya kimfumo ambayo imekuwa ikiendelea kwa miaka mingi imefichua uongo wa madai ya “uvumilivu na kuheshimu dini” yanayotangazwa na serikali. Hali imefikia kiwango kwamba wafuasi wa dini zisizo za Kiislamu, na hata makafiri na washirikina, wamekuwa na mazingira bora zaidi kuliko Waislamu na wananchi wa asili wa nchi hiyo.

Wanazuoni wa Bahrain walilaani uvamizi huu wa kidhalimu na wakataka usimamishwe mara moja, pamoja na kuachwa kwa sera ya uchochezi na ya kuvuruga utulivu wa msimu wa Ashura.

Walisisitiza kwamba; kuheshimu uhuru wa kidini na kuruhusu Waumini kuhuisha maombolezo yao ya Husseini ni haki ya msingi ambayo haipaswi kukiukwa kwa sababu yoyote ile.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha