Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Ahmad Safi, msimamizi wa kisheria wa Haram Takatifu ya Abbasiyya na mwakilishi wa Ayatullah al-Udhma Sistani, wakati wa kumpokea Hujjatul-Islam wal-Muslimin Ridha Ramadhani, Katibu Mkuu wa Majma' al-'Alami li-Ahlil-Bayt, pamoja na ujumbe aliokuwa ameandamana nao, alisisitiza kwamba; shughuli za tablighi ni jukumu linalowahusu wote na zina athari ya kina katika muundo wa jamii.
Katika mkutano huo, walijadiliana kuhusu masuala mbalimbali ya kitamaduni na tablighi, pamoja na njia za kuimarisha ushirikiano wa kitamaduni na kimedia kati ya taasisi husika kwa lengo la kuitumikia fikra halisi ya Kiislamu.
Mwakilishi wa Ayatullah Sistani, akirejelea umuhimu wa kuelewa hali halisi ya sasa na mazingira ambayo jamii za Kishia zinapitia kwa kuzingatia tajriba za kihistoria, na akitolea mfano matukio ya zama za Hadhrat Amirul-Mu’minin na Hadhrat Fatimah al-Zahra (as), aliongeza kuwa; misimamo hiyo ina mafunzo na mazingatio ambayo yanaweza kutumiwa katika kukabiliana na changamoto za kisasa.
Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Safi alipendekeza kwamba; mikutano ya aina hii itumike kuzindua programu za kitamaduni na kielimu zinazowalenga vijana, hususan wanafunzi wa vyuo vikuu.
Pia alisisitiza umuhimu wa kunufaika na matukio na programu mbalimbali, ikiwemo sherehe za kuhitimu masomo na hafla za kula kiapo mbele ya Imam Ridha (as), kwa kuwa programu hizi zina athari kubwa chanya katika hali ya kisaikolojia ya wahitimu na huchangia katika kukabiliana na changamoto za kiakili na kitamaduni za zama hizi.
Msimamizi wa kisheria wa Haram ya Hazrat Abbas (as) mwishoni alisisitiza kwamba; madrasah ya Imam Hussein (as) katika historia yote imekuwa daima sababu yenye athari kubwa katika kuleta mabadiliko chanya na kuvuruga mipango ya maadui.
Aidha, alisisitiza umuhimu wa shughuli za tablighi na kuongeza kwamba; kila mtu kulingana na nafasi yake ana wajibu katika uwanja huu, kwa sababu shughuli hizi zina mchango mkubwa na wa msingi katika kuijenga jamii.
Maoni yako