Alhamisi 11 Juni 2026 - 16:15
Msemaji wa Hamas: Iran Inajitahidi Kusitisha Vita vya Ghaza

Hawza/ Hazem Qassem, msemaji wa Harakati ya Hamas, amesema kwamba: Iran imeifikishia harakati hiyo juhudi zake za kidiplomasia za kumaliza migogoro katika eneo, ikiwemo vita vya Ghaza.

Kwa mujibu wa Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, likinukuu Islami Analysis, Hazem Qassem, msemaji rasmi wa Hamas, alisema kwamba; Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa ikiishirikisha harakati hiyo juhudi zake za kidiplomasia za kumaliza vita katika nyanja mbalimbali, ikiwemo Ghaza. Pia alitoa ujumbe muhimu kuhusu mazungumzo ya usitishaji vita na msaada wa washirika wa mhimili wa muqawama katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa ripoti ya Al Mayadeen, Qassem, akisisitiza kwamba; Iran inauunga mkono muqawama wa Palestina kisiasa, kijeshi na kifedha, alisema kuwa Tehran inaendelea kuonesha mshikamano na kuwaunga mkono wananchi wa Palestina.

Alisema: "Sisi ndani Hamas tunajitahidi kuhakikisha kwamba; mshikamano wa kikanda pia unaijumuisha Ghaza, na kwamba Ukanda wa Ghaza unabaki kuwa kitovu cha mlinganyo wa kikanda; mlinganyo ambao lengo lake ni kusimamisha mashambulizi na kumaliza vita."

Msemaji wa Hamas aliendelea kwa kuashiria mazungumzo yanayoendelea mjini Cairo na kusema kwamba; harakati hiyo bado imeacha milango ya mazungumzo na suluhisho la kisiasa wazi.

Aliongeza: "Sisi kama harakati tuna mtazamo chanya kwa ombi lolote la kimantiki litakalowasilishwa mjini Cairo, na tunatumai kufikia suluhisho za kudumu katika muda mfupi iwezekanavyo. Hamas imeazimia kikamilifu kuharakisha mchakato wa kufikia makubaliano yatakayositisha vita vya mauaji ya kimbari huko Ghaza, kupunguza mateso ya wananchi na kukomesha mashambulizi yanayoendelea."

Katika sehemu ya mwisho ya matamshi yake, Qassem alizungumzia mashambulizi ya Israel dhidi ya Lebanon na mwitikio wa vikosi vya mhimili wa muqawama, akisema kwamba; Hamas inashukuru sana" majibu ya kijeshi ya Iran na Yemen kwa matukio hayo.

Kisha aliuhutubia ulimwengu wa Kiislamu kwa kusema: "Mwelekeo huu ni mfano halisi wa mshikamano kati ya sehemu mbalimbali za Umma wa Kiislamu. Tunaziomba nguvu hai na zenye athari za Umma wa Kiislamu kuzingatia kiwango hiki cha mshikamano na wananchi wa Palestina na Lebanon kuwa wajibu mkuu na wa dharura wa kipindi hiki cha kihistoria."

Msemaji wa Hamas alihitimisha kwa kusisitiza umuhimu wa kuimarisha uungaji mkono wa kisiasa na wa wananchi kwa Palestina na Lebanon, na akatoa wito wa kupanuliwa kwa ushirikiano na mshikamano kati ya nchi za Kiislamu katika kukabiliana na migogoro inayoendelea katika eneo hilo.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha