Alhamisi 4 Juni 2026 - 14:00
Kongamano la uhamasishaji kuhusu mafanikio ya Imam Khomeini (r.a.) nchini Nigeria

Hawza/ Katika mwendelezo wa ratiba za wiki ya kumbukumbu ya Imam Khomeini (r.a.), Jukwaa la Wasomi wa Vyuo Vikuu na Wahadhiri (Academic Forum) la Harakati ya Kiislamu chini ya uongozi wa Sheikh Ibrahim Zakzaky, limeandaa programu ya kuelezea na kutoa mwamko kuhusu mafanikio na huduma za Imam Khomeini (r.a.) kwa ulimwengu wa Kiislamu.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, katika mwendelezo wa mikutano na hafla za wiki ya kumbukumbu ya Imam Khomeini (r.a.), Jukwaa la Wasomi wa Vyuo Vikuu na Wahadhiri wa Harakati ya Kiislamu chini ya uongozi wa Sheikh Ibrahim Yaqub Zakzaky, tawi la Jimbo la Katsina, limeandaa kongamano kwa lengo la kutoa mwamko, kutambulisha shakhsia ya Imam Khomeini na kuelezea nafasi yake ya kudumu katika kuinua dini tukufu ya Uislamu.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wanachama wa jukwaa hilo walifika katika maeneo mbalimbali ya mji, hususan katika Msikiti Mkuu wa eneo hilo, na wakawaelezea wananchi kwa ujumla juhudi na huduma muhimu za Imam Khomeini (r.a.) kwa Uislamu.

Katika programu hiyo ya uhamasishaji walisisitiza kwamba; Imam Khomeini (r.a.) hakuwa tu kiongozi wa nchi maalumu, bali alikuwa kiongozi wa ulimwengu wa Kiislamu na wa waliodhulumiwa; mtu ambaye aliwafundisha watu wote namna ya kusimama dhidi ya dhulma na ubeberu, na jinsi ya kufanya juhudi kwa ajili ya kusimamisha serikali ya Kiislamu (kwa msingi wa kanuni ya Wilayat al-Faqih).

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha