Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, kusini mwa Lebanon tangu usiku wa manane wa Jumamosi hadi Jumapili kumeshuhudiwa mfululizo wa mashambulizi makubwa ya Israel yaliyohusisha mashambulizi ya anga, mashambulizi ya mizinga pamoja na mashambulizi ya ndege zisizo na rubani. Mashambulizi haya yalilenga idadi kubwa ya miji na vijiji vya kusini na yalisababisha watu kadhaa kuuawa na kujeruhiwa, sambamba na uharibifu mkubwa wa mali.
Ndege za kivita za Israel zilifanya mashambulizi kadhaa katika kitongoji cha “Al-Arab” katika mji wa “Deir al-Zahrani” na zililenga nyumba za makazi zilizoko karibu na jengo la manispaa, jambo lililosababisha kutendeka jinai kubwa ambayo iliacha idadi ya mashahidi na majeruhi, wakiwemo baadhi ya wanachama wa kabila la “Al-Karidin.”
Vikosi vya uokoaji na ulinzi wa kiraia vinaendelea na operesheni za kutafuta na kuwatoa wahanga waliokwama chini ya vifusi, ripoti pia zinaonyesha kuwepo kwa idadi kubwa ya majeruhi kufuatia mashambulizi yaliyolenga mji huo.
Mashambulizi haya ya anga yalienea hadi katika miji ya “Al-Nabatiyah,” “Kafr Tabnit,” “Shoukin,” “Kafr Rumman,” “Mifdoun,” “Arab Salim,” “Arnoun,” “Yahmar al-Shaqif,” “Al-Ghanduriyah,” “Deir Qanoun al-Nahr,” pamoja na maeneo yanayozunguka hospitali ya “Hiram” katika mji wa Tyre.
Aidha, ndege isiyo na rubani ya adui ililenga pikipiki katika mji wa “Al-Qusaybah”, jambo lililosababisha kujeruhiwa kwa raia wawili wa Syria, na baada ya hapo ndege ya kivita ya adui pia ililenga mji huo, vilevile, ndege nyingine isiyo na rubani ya adui ililenga maeneo ya karibu na maonesho ya Ulaya katika barabara kuu ya “Habboush–Zahrani”, huku ndege nyingine ikifanya shambulizi katika maeneo ya karibu ya mji wa “Al-Sharqiyah.”
Katika shambulizi jingine, ndege isiyo na rubani ya Israel iliwalenga wafanyakazi kadhaa wakati wa kuvuna matikiti maji katika shamba lililopo pembezoni mwa mji wa “Burj al-Shamali,” hata hivyo hakuna hasara za maisha zilizoripotiwa.
Sambamba na mashambulizi haya, maeneo mengi pia yalilengwa kwa mashambulizi ya mizinga ya Israel, yakiwemo maeneo ya karibu na mto “Litani” karibu na daraja la “Al-Dalafah,” pamoja na mji wa “Kafr Rumman” na eneo la “Kafr Jouz” katika wilaya ya “Al-Nabatiyah.”
Jeshi la uvamizi la Israel pia lilifanya operesheni ya kubomoa nyumba katika mji wa “Dibbin” katika wilaya ya “Marjeyoun,” jambo ambalo lilifanyika sambamba na mashambulizi mawili ya anga yaliyolenga maeneo ya karibu ya mji huo.
Kuongezeka huku kwa mvutano kunafanyika katika muktadha wa kuendelea kwa mashambulizi ya Israel dhidi ya maeneo ya kusini, huku kukiwa na safari nyingi za ndege za kivita na ndege zisizo na rubani zinazopaa juu ya vijiji na miji kadhaa iliyolengwa.
Maoni yako