Jumanne 2 Juni 2026 - 13:34
Bendera ya Hadithi ya Ghadir kupeperushwa Katika Haram ya Qamar Bani Hashim

Hawza/ Kamati ya wahudumu wa Haram ya Hadhrat Abbas (as), imepokea bendera ya Hadithi ya Ghadir kutoka kwa Bodi ya Wadhamini wa Haram Tukufu ya Alawi, kwa ajili ya kufungwa katika eneo maalumu.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, ujumbe uliowasili kutoka Haram ya Imam Ali (as) ulipokelewa na wajumbe wa bodi ya uongozi ya Ataba Tukufu, akiwemo Dkt. Afdhal Al-Shami pamoja na mkuu wa Idara ya Mahusiano ya Umma wa Ataba hiyo, Bw. Muhammad Ali Adhhar.

Bw. Al-Shami katika hafla hiyo alieleza: “Waheshimiwa kutoka Haram Tukufu ya Imam Ali (as) walitupa heshima ya kuitembelea Haram ya Aba al-Fadhl al-Abbas (as), na walitukabidhi bendera ya Ghadir ambayo kila mwaka hupeperushwa kwenye Haram Tukufu za Ahlul-Bayt (as) kwa mnasaba wa Idi ya Ghadir.”

Aliongeza kwamba; bendera ya Ghadir itapeperushwa katika Haram Tukufu ya Aba al-Fadhl al-Abbas (as) katika eneo ambalo litabainishwa baadaye, ili kushiriki na kushirikiana na Haram Tukufu ya Imam Ali (as) katika kuadhimisha mnasaba huu wenye baraka.

Chanzo: Al-Kafeel.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha