Ijumaa 29 Mei 2026 - 17:00
Vatican Yaingia Katika Mjadala wa Akili Mnemba; Papa Leo wa Kumi na Nne Aonya Kuhusu Ukiritimba wa Teknolojia

Hawza/ Waraka wa kwanza wa Kanisa uliotolewa na Papa Leo wa Kumi na Nne umejikita katika suala la akili mnemba (AI) na umeonya kuhusu mkusanyiko wa nguvu za kiteknolojia mikononi mwa kampuni chache kubwa duniani, matumizi ya kijeshi ya akili mnemba pamoja na kuongezeka kwa ufuatiliaji na udhibiti wa kidijitali kwenye jamii.

Shirika la Habari la Hawza – Vatican kwa kuchapisha waraka wa kwanza wa Kanisa wa Papa Leo wa Kumi na Nne, imeingia rasmi katika mjadala wa kimataifa kuhusu akili mnemba na athari zake za kimaadili na kijamii.

Waraka huo uliotolewa kwa jina la “Magnifica Humanitas” (Utukufu wa Ubinadamu), umesisitiza umuhimu wa kuhifadhi heshima ya mwanadamu katika zama za akili mnemba na umeonya kuhusu athari za kisiasa, kiuchumi na kitamaduni za teknolojia mpya.

Katika waraka huu, kumeoneshwa wasiwasi kuhusu mkusanyiko wa data, miundombinu ya kidijitali na algorithimu mikononi mwa idadi ndogo ya kampuni kubwa za teknolojia.

Papa Leo wa Kumi na Nne amesisitiza kwamba; teknolojia na algorithimu si vitu visivyoegemea upande wowote, bali mara nyingi huathiriwa na maslahi ya kiuchumi na kisiasa ya wamiliki wake, pia katika waraka huu imeonywa kwamba; mustakabali wa kidijitali wa dunia haupaswi kuwekwa mikononi mwa vituo vichache vya nguvu na utajiri.

Sehemu nyingine ya waraka huu wa Kanisa imehusu matumizi ya kijeshi ya akili mnemba. Papa katika kauli zake ametaka matumizi ya kijeshi ya akili mnemba yadhibitiwe, na ameonya kuhusu maendeleo ya mifumo ya kivita inayotegemea, teknolojia za ufuatiliaji na kuigeuza akili mnemba kuwa chombo cha utawala wa mabavu na vita.

Pia katika waraka huu kumeoneshwa wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa udhibiti wa kijamii, kuchezewa kwa fikra za umma na kusambazwa kwa taarifa za kupotosha kupitia teknolojia mpya.

Vatican katika waraka huu imesisitiza kwamba; suala la akili mnemba si tu mada ya kiufundi, bali linahusiana na uadilifu wa kijamii, heshima ya mwanadamu na mustakabali wa jamii za kibinadamu.

Katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na kuongezeka kwa ushawishi wa kampuni kubwa za teknolojia na kusambaa kwa akili mnemba katika nyanja za kiuchumi, kiusalama na vyombo vya habari, mjadala kuhusu udhibiti na usimamizi wa teknolojia hii umegeuka kuwa moja ya masuala muhimu duniani.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha