Kwa mujibu wa kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Shule ya Qur’ani ya Nur ambayo ipo ndani ya msikiti uliobomoka kwa kiasi kikubwa, imegeuka kuwa kimbilio la mamia ya watoto na wanawake wakimbizi walioathiriwa na vita, kupoteza wapendwa wao na kukosa makazi, ambao wameikimbilia shule hiyo. Wanafunzi hukusanyika kila siku kusoma Qur’ani na kuihifadhi, kujifunza mafundisho ya dini, na kupata utulivu wa kihisia baada ya miaka ya vurugu, njaa na kupoteza hisia za usalama.
Wengi wa wanaojifunza Qur’ani wanasema kuwa; shule hii imewasaidia kukabiliana na majeraha yaliyotokana na kupoteza nyumba zao na wapendwa wao.
Huda Al-Farah, mmoja wa wanafunzi wa Qur’ani, alisema kuwa; familia yake ilipoteza nyumba yao wakati wa vita na walilazimika kuishi katika hema, lakini kukimbilia Qur’ani kuliwapa nguvu ya kuendelea kuwa na subira na kusonga mbele.
Rasha Al-Far, mmoja wa wanafunzi wa Qur’ani mwenye umri wa miaka kumi na nne, alieleza namna vita vilivyobadilisha maisha yake kutoka hali ya utulivu hadi kukosa makazi na kuingia katika hali kubwa ya kunyimwa mahitaji muhimu, alisema kuwa; alijiunga pamoja na mama yake katika Shule ya Qur’ani ya Nur ili wapate utulivu katikati ya matatizo yanayowazunguka.
Rami Al-Shaker, mkuu wa Kituo cha Hifdh na Sayansi za Qur’ani cha Nur, alisema kuwa; shule hiyo ilianzishwa kwa lengo la kusaidia uponaji wa kisaikolojia na kufundisha mafundisho ya Qur’ani kwa Wapalestina baada ya vita, mbali na kuhifadhi Qur’ani, kituo hicho pia kinatoa programu za ushauri nasaha na msaada wa kihisia chini ya usimamizi wa wataalamu wa fani hiyo.
Chanzo: Shirika la Karbala Now Agency
Maoni yako