Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, wafungwa walikuwa wakikumbuka kumbukumbu ya shahada ya Imam Jawad (as), Imam wa tisa wa Mashia, ambayo huadhimishwa katika siku ya ishirini na tisa ya mwezi wa Qamari wa Dhul-Qa'dah, wakati walinzi wa gereza walipovamia jengo walilokuwa wamezuiliwa na kuanza kuwapiga waombolezaji, tukio hili liliripotiwa na kituo cha televisheni cha Kiarabu cha Luluwa TV.
Baada ya kuwapiga wafungwa hao, vikosi vya utawala wa kifalme wa Bahrain viliwaweka katika vizimba vya upweke, Utawala huo pia umewafunga mamia ya raia wa Bahrain katika gereza maarufu la "Jela ya Jaw", kwa kosa la kushiriki katika mikusanyiko ya amani inayounga mkono demokrasia nchini Bahrain.
Maelfu ya wafuasi wa demokrasia nchini Bahrain wanaopinga utawala wa kifalme wamekuwa wakifanya mikusanyiko ya amani kila siku mara kwa mara tangu katikati ya mwezi Februari mwaka 2011.
Manama imechukua hatua kubwa za kukandamiza harakati zozote zinazodai demokrasia, tarehe 14 Machi 2011, vikosi kutoka Saudi Arabia na Falme za Kiarabu vilitumwa nchini Bahrain kwa lengo la kuisaidia serikali ya Bahrain katika kukabiliana na maandamano ya wananchi wake.
Chanzo: Al-Ahed News.
Maoni yako