Jumanne 26 Mei 2026 - 09:00
Yeyote Atakaye Kubaliana na Mipango ya Sasa ya Adui Mzayuni Atakuwa Mshirika Mkuu Katika Kumwaga Damu za Mashahidi

Hawza/ Rami Abou Hamdan alisema: Kinachoendelea leo ni zaidi ya madai ya kujaribu kufanikisha usitishaji vita kupitia makubaliano dhaifu; bali ni juhudi za kuisukuma Lebanon kuelekea kwenye “uanzishaji wa uhusiano wa kiusalama wa kawaida” na adui.

Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Rami Abou Hamdan, mbunge wa Lebanon na mwanachama wa Kundi la “Uaminifu kwa Muqawama”, katika hafla ya mazishi ya shahidi mujahidi Wakili Ali Abou Zeid, iliyoandaliwa na Hizbullah pamoja na wafuasi wa Muqawama katika mji wa Ali al-Nahri katika eneo la Biqaa, alisisitiza kwamba; kinachoendelea leo ni zaidi ya madai ya kujaribu kufanikisha usitishaji vita kupitia maelewano dhaifu; bali ni juhudi za kuisukuma Lebanon kuelekea kwenye “uanzishaji wa uhusiano wa kiusalama wa kawaida” au kuunda “ukanda wa kiusalama wenye utata”.

Alionya kwamba, hatua hii ya “uanzishaji wa uhusiano wa kiusalama wa kawaida” ni sawa na tangazo la vita ndani ya nchi, na akasisitiza kwamba ni uongozi huu wa kisiasa, kwa vipengele vyake vyote unaotishia uwepo wa Lebanon, nafasi yake na wajibu wake.

Abou Hamdan alieleza kwa msimamo thabiti kwamba; kuelekea kwenye aina yoyote ya njia au makubaliano ya kiusalama na adui wa jadi, yaani Israel, kwa jina lolote au chini ya anuani yoyote ile, ni jambo ambalo haliwezi kudhibitiwa wala kukubalika kisiasa kwa namna yoyote.

Mwanachama huyo wa Kundi la Muqawama alikumbusha kwamba: Yeyote atakaye kubaliana na mipango ya sasa ya adui Mzayuni, atahesabiwa kuwa mshirika mkuu katika kumwaga damu za mashahidi, wapiganaji wa jihadi, watoto na wanawake.

Mbunge huyo wa Lebanon pia alisisitiza kwamba; damu za mashahidi zitaendelea kuwa na thamani kubwa zaidi kuliko nyadhifa na viti vya mamlaka, na kwamba juhudi zote za kulazimisha maagizo na masharti haya zitashindwa na hazitafanikiwa.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha