Ijumaa 22 Mei 2026 - 10:40
Mgomo wa pamoja nchini Italy

Hawza/ Italia wiki hii imeshuhudia mgomo wa kitaifa uliogusa sekta za usafiri, elimu na usafirishaji wa bidhaa, mgomo huu ulifanyika kufuatia wito wa vyama vya wafanyakazi kwa lengo la kupinga mipango ya kujiimarisha kijeshi, kulaani mauaji ya kimbari yanayoendelea yanayofanywa na utawala wa Israel huko Ghaza, na kuonesha mshikamano na “Msafara wa Sumud” ambao unajaribu kuvunja mzingiro wa Ukanda wa Ghaza.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, mgomo huu uliambatana na maandamano katika miji kadhaa ya Italia, ambapo wananchi walipaza sauti kauli mbiu ya “Simamisheni jambo hili”, maandamano ambayo yaliandaliwa na vyama vya wafanyakazi na makundi ya kiraia kwa lengo la kupinga kuongezeka kwa matatizo ya maisha, sera za kijeshi na kuongezeka kwa bajeti ya silaha kwa gharama ya huduma za afya na elimu. Pia walitaka kukomeshwa kwa mauaji ya kimbari dhidi ya wananchi wa Palestina na kuungwa mkono kwa Msafara wa Sumud unaoelekea Ghaza.

Katika mji wa Rome, waandamanaji walikusanyika katika moja ya viwanja vikuu vya mji huo, na kwa kubeba mabango yaliyoitaka serikali ya Italia isiendelee na “ushiriki katika jinai” pamoja na Israel.

Miongoni mwa washiriki alikuwapo mwanaharakati Mhispania-Mpalestina, Saif Abu Kishk, mmoja wa wanaharakati waliokamatwa wakati wa shambulio la Israel la tarehe 29 Aprili dhidi ya msafara huo katika maji ya kimataifa karibu na kisiwa cha Crete.

Chanzo: Palinfo English

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha