Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, kwa lengo la kuenzi kumbukumbu na historia ya mashahidi wa shule ya “Shajarat Tayyibah Minab”, mashindano yaliyopewa anuani ya “Wito wa Amani na Ubinadamu; mashindano baina ya shule mbalimbali” yalifanyika kwa ushiriki wa kundi la wanafunzi na watu waliovutiwa, kwa juhudi za kituo cha ushauri wa kitamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Rawalpindi na kwa ushirikiano na Chama cha Usimamizi wa Shule Binafsi cha Punjab Kaskazini nchini Pakistan, katika mji wa Rawalpindi, Pakistan.
Lengo kuu la programu hii lilikuwa kutoa heshima na kuwaenzi wanafunzi mashahidi wa shule ya “Shajarat Tayyibah Minab” ambao waliuawa kishahidi katika shambulio la makombora la Marekani na utawala wa Kizayuni. Vilevile katika hafla hii ilisisitizwa haja ya kueneza ujumbe wa amani, mshikamano wa kibinadamu na kuunga mkono haki za watoto duniani kote.
Katika mashindano haya ya hotuba, wanafunzi katika hotuba zao walisisitiza kwamba; watoto hawapaswi kamwe kuwa wahanga wa vita na migogoro, na kwamba kuandaa mazingira salama, yenye utulivu na yanayofaa kwa elimu yao ni jukumu la pamoja la jamii ya kimataifa.
Washiriki walionesha masikitiko yao makubwa na kusema: Nchi kama Marekani na utawala wa Kizayuni, kwa ajili ya kufikia malengo yao ya kisiasa na kimkakati, hufanya vitendo ambavyo matokeo yake ni kuuawa watu wasio na hatia, hasa watoto.
Waliohudhuria huku wakitangaza mshikamano wao na familia pamoja na wanafunzi mashahidi wa shule ya “Shajarat Tayyibah Minab”, walilaani vikali tukio hilo na kutaka wahusika wake wafikishwe katika vyombo vya kimataifa vya haki kwa ajili ya kuhukumiwa kwa uadilifu.
Katika hafla hiyo, Mahdi Taheri, mkuu wa Nyumba ya Utamaduni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Rawalpindi, alisema katika hotuba yake: “Jamhuri ya Kiislamu ya Iran siku zote imekuwa ikipinga vita na vurugu, lakini kamwe haitasalimu amri mbele ya dhulma na ukosefu wa haki, taifa la Iran daima limesisitiza kutembea katika njia ya haki na uadilifu na limesimama kidete mbele ya mabavu na udikteta.”
Inafaa kutajwa kuwa; mashindano hayo yalifanyika katika sehemu tatu, na wanafunzi walitoa hotuba zao kwa lugha za Urdu na Kiingereza, mwishoni, watu watatu bora katika kila sehemu walitunukiwa zawadi na vyeti vya pongezi.
Maoni yako