mujibu wa Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Sayyid Yasin Mousawi, Imam wa Swala ya Ijumaa wa Baghdad na mmoja wa walimu mashuhuri wa Hawza ya Najaf, katika khutba za Swala ya Ijumaa (18 Ordibehesht 1405 / 8 Mei 2026), alitangaza kwamba; mwenendo wa kisiasa nchini Iraq kutokana na baadhi ya mikondo ya kisiasa kujitenga na matakwa ya wapiga kura, unakabiliwa na changamoto hatari.
Alisisitiza kwamba; ushiriki wa wananchi katika uchaguzi ulifanyika kwa lengo la kuhifadhi mwendelezo wa njia ya kidemokrasia na kuzuia kuporomoka kwa nchi, lakini namna ya kusimamia medani ya kisiasa baada ya uchaguzi imesababisha kuibuka kwa hali ya kukata tamaa miongoni mwa maoni ya umma.
Ayatullah Mousawi aliongeza kuwa: Pingamizi lake halielekezwi kwa watu binafsi, bali linahusiana na hatima ya Iraq na mustakabali wa mfumo wa kisiasa. Alionya kwamba; kutoyajali matakwa ya wananchi na kutekeleza matwakwa ya raia kwa kiburi kunaweza kuipeleka nchi kwenye mlipuko hatari wa kijamii.
Imam wa Swala ya Ijumaa wa Baghdad alisisitiza kwamba; maraji' wa dini na wenye hekima wa Iraq daima wamejaribu kudhibiti hasira za umma ili nchi isiingie katika machafuko.
Pia kuhusu nafasi ya marjaiya ya dini katika kipindi kilichopita alisema: Marjaiya ilifanya juhudi kubwa za kutoa nasaha na miongozo kwa mikondo ya kisiasa, lakini mwishowe ilifikia hitimisho kwamba; wanasiasa wengi hawazingatii ushauri huo. Kwa hiyo, marjaiya ilipunguza kiwango cha kuingilia kwake moja kwa moja katika maingiliano na tabaka la kisiasa, ingawa imeacha wazi mlango wa uongofu na maelekezo kwa wale wanaotafuta mageuzi.
Ayatullah Mousawi katika sehemu nyingine ya hotuba yake huku akirejelea mabadiliko ya kimataifa, alisema kwamba; dunia tangu kumalizika kwa vita ya II ya dunia hadi sasa imeshuhudia mabadiliko makubwa katika mizania ya nguvu, na mfumo wa kimataifa ulioundwa baada ya vita hivyo sasa uko katika hali ya kuporomoka kutokana na kuibuka kwa nguvu mpya kama China na kubadilika kwa mifumo ya jadi ya miungano.
Aliongeza kwamba; nchi nyingi, chini ya kivuli cha migogoro inayoongezeka ya kisiasa, kiuchumi na kiusalama, zinajaribu kufafanua upya nafasi zao katika mfumo mpya wa dunia.
Imam wa Swala ya Ijumaa wa Baghdad pia alizungumzia mabadiliko ya kikanda na kuzungumzia mvutano unaoongezeka kati ya Iran na Marekani pamoja na juhudi za Washington za kulazimisha utawala wake katika eneo. Alisema kwamba; baadhi ya mikondo ya kisiasa ya eneo hili inafuata mkakati wa “kutokuegemea upande wowote” na kutegemea msaada wa Marekani, huku mkondo mwingine ukisisitiza uhuru wa maamuzi ya kitaifa na kuondoka kwa majeshi ya kigeni kutoka Iraq.
Ayatullah Mousawi alisisitiza kwamba; Iraq ina uwezo wa kihistoria na wa kibinadamu unaohitajika kwa ajili ya kuwa nchi yenye nafasi ya msingi katika eneo hili, na akakosoa kushughulika kwa mikondo ya kisiasa na migogoro kuhusu nyadhifa na wizara badala ya kushughulikia mafaili ya ufisadi, ukosefu wa ajira na kushuka kwa huduma za umma. Kwa mujibu wake, kuendelea kwa hali hii kutaifanya Iraq ibaki katika mzunguko wa udhaifu na utegemezi wa kigeni.
Mwalimu wa Hawza ya Najaf katika sehemu nyingine ya khutba yake alisifu uimara wa vikosi vya Muqawama nchini Lebanon na kusema kwamba; kusimama imara kwa msingi wa wananchi wa Muqawama katika nchi hiyo kunaonesha kushikamana kwao na chaguo la Muqawama licha ya mashinikizo ya kisiasa na kijeshi.
Pia aliongeza kwamba mataifa ya eneo hili yanafuatilia kwa makini mabadiliko yanayohusiana na mvutano wa kikanda, hasa mazungumzo na makabiliano kati ya Tehran na Washington.
Imam wa Swala ya Ijumaa wa Baghdad mwishoni mwa khutba yake alisisitiza kwamba; mataifa yenye uelewa yana uwezo wa kujenga mustakabali wao na kulinda mamlaka yao ya kitaifa, na akawataka wanasiasa wa Iraq kupitia upya misimamo yao na kujitahidi kujenga nchi yenye nguvu, huru, inayojibu matakwa ya wananchi na inayolinda heshima ya taifa.
Maoni yako