Alhamisi 30 Aprili 2026 - 11:30
Balozi mdogo wa Iran mjini Istanbul: Iran imewaangusha mafirauni wa zama hizi

Hawza/ Taasisi 14 za vijana zilizoko Istanbul ziliandaa programu ya pamoja katika ukumbi wa Kadir Topbaş na kutangaza mshikamano wao na Iran; programu iliyohudhuriwa na balozi mdogo wa Iran na ushiriki mpana wa wanaharakati wa kitamaduni na wananchi, ikiwa ni taswira ya umoja na mshikamano.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, ukumbi wa Kadir Topbaş unaomilikiwa na manispaa ya Bağcılar ulikuwa mwenyeji wa tukio muhimu lililolenga mshikamano, lililoandaliwa kwa juhudi za taasisi za vijana wa Istanbul.

Programu hii, iliyofanyika kwa mfumo wa ukusanyaji wa misaada ya wananchi kwa lengo la kuiunga mkono Iran, ilishuhudia ushiriki wa makundi 14 ya vijana na kuonesha kwa namna yenye maana hali ya umoja na mshikamano.

Katika programu hii, taasisi mbalimbali zilishiriki, zikiwemo: Jumuiya ya Elimu na Utamaduni ya “Matumaini ya Vijana”, Kituo cha Maudhui cha “Mektebi”, Kundi la Vijana la Huda Ahlul-Bayt, Jukwaa la Uhamasishaji, Jumuiya ya Muhammad Mustafa, Vijana wa Msikiti wa Abu Talib, “Nurul Islam”, “Penah Tur”, Chapisho la “Palmiye”, “Mektep Pusulası”, Kituo cha Wanawake “Kevser”, “Tükenmez Gençlik”, “Hel Eta 313” na Vijana wa Ahlul-Bayt wa Uturuki.

Programu ilianza kwa usomaji wa aya za Qur’ani Tukufu uliotekelezwa na Oghuzhan Uluç, na kisha Zaynab Otay kwa niaba ya waandaaji, aliwakaribisha waliohudhuria na kusisitiza umuhimu wa mshikamano wa vijana, akiuona kuwa “mfano bora wa harakati kuelekea lengo la pamoja.”

Taner Korhan, msimamizi wa programu, pia alisisitiza umuhimu wa kuunga mkono kizazi cha vijana akisema: “Ni lazima tushike mikono ya vijana hawa na kueneza sauti yao katika vyombo vyote vya habari na mitandao ya televisheni.”

Katika programu hii, Ahmad Mohammadi, balozi mdogo wa Iran mjini Istanbul pia alihudhuria. Akiwa ameathiriwa na baadhi ya sehemu za hafla na kukumbuka mashahidi wa Minab, alisema: “Iran kwa mashahidi wake wote imewapiga chini mafirauni wa zama.”

Vilevile, Nureddin Şirin, mkurugenzi mkuu wa mtandao wa Quds, katika hotuba yake alisisitiza umuhimu wa kuchukua msimamo kwa uelewa huku akisema: “Suala ni kubainisha safu na kuchukua msimamo,” na akapongeza mwenendo wa vijana.

Katika sehemu nyingine ya programu, Izzat Jaf alisoma dua ya mwisho. Katika baadhi ya vipengele vya hafla, baadhi ya watoto walionesha kuiunga Iran kwa kuchana bendera za Marekani na Israel pamoja na picha za Donald Trump na Benjamin Netanyahu juu ya jukwaa.

Zaynab Otay katika mahojiano na Shirika la Habari la Hawza, akirejea mapokezi makubwa ya wananchi kwa programu hii, alitangaza kwamba; mwishoni mwa hafla, misaada iliyokusanywa ilikabidhiwa kwa ubalozi mdogo wa Iran mjini Istanbul ili itumwe Iran.

Inafaa kutajwa kuwa programu hii ilichochea hasira za Mossad, shirika la ujasusi la utawala wa Kizayuni, na kufuatia hilo shirika hilo lilitoa malalamiko yake kupitia ujumbe katika mtandao wa X.

Mossad katika majibu yake iliandika: Hapana, hapa si Iran. Hii ni Uturuki, mwanachama wa NATO. Katika hafla iliyofanyika Uturuki kwa ajili ya kuwakumbuka wahanga wa shambulio la shule ya Minab, watoto waliombwa kuchana juu ya jukwaa picha za Donald Trump rais wa Marekani, Benjamin Netanyahu waziri mkuu wa Israel pamoja na bendera za Marekani na Israel. Katika mandharinyuma pia kulikuwa na picha ya (Ayatullah Sayyid) Ali Khamenei, kiongozi wa zamani wa Iran, ikionyeshwa kwa uwazi. Je, Uturuki inachukua nafasi ya Iran kama kituo kipya cha muqawama? Hatima ya watoto hawa katika miaka 15 ijayo itakuwaje?

Mlango wa Hormuz utabakia milele chini ya mamlaka na udhibiti wa Iran/ Mzingiro wa baharini kwetu ni jambo la kuchekesha

Mlango wa Hormuz utabakia milele chini ya mamlaka na udhibiti wa Iran/ Mzingiro wa baharini kwetu ni jambo la kuchekesha

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha