Kwa miongo kadhaa, mataifa ya Afrika yameonja uchungu wa ukoloni, Wakoloni hawakuiba rasilimali zao tu, bali pia walilenga utambulisho wao wa kitamaduni, lugha zao, na uhuru wao wa fikra. Hadi leo, athari za enzi hizo zinaonekana katika miundo mingi ya kisiasa na kiuchumi ya nchi mbalimbali za Afrika. Hata hivyo, dhidi ya historia hii iliyojaa maumivu, roho ya upinzani na uongozi wa kutafuta uhuru wa watu wa bara hili haijawahi kuzimwa, wala haitazimika.
Katika miongo ya hivi karibuni, Iran imekuwa mfano mpya kwa mataifa yanayotaka kusimama kwa miguu yao wenyewe. Nchi ambayo, licha ya shinikizo, vikwazo na vitisho, iliamua badala ya kutegemea nguvu za mataifa makubwa, kujiamini na kuwa na matumaini kwa uwezo wa watu wake. Ujasiri huu—si tu uwanjani mwa siasa, bali pia katika sayansi, teknolojia, na utamaduni—umeonekana. Iran imeonyesha kuwa “uhuru” si kauli tu, bali ni namna ya kujijenga, kujiamini, na imani kwenye haki.
Kwa watu wengi wa Afrika, uzoefu wa Iran unawakumbusha ukweli huu: inawezekana kusimama dhidi ya ukandamizaji, bila kujisalimisha kwa hofu au udanganyifu.
Iran na mataifa ya Afrika hukutana kwenye thamani ya pamoja: nayo ni "kuamini heshima ya binadamu na haki ya kuchagua hatima yao wenyewe".
Maoni yako