Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, hafla ya upandishaji wa Bendera ya Imam Hussein (as) iliyofanyika jijini humo kwa kuandaliwa na Taasisi ya Ahlulbayt Center pamoja pamoja na Husseiniya ya Zainabiyya, iliashiria rasmi kuanza kwa majlisi na shughuli mbalimbali za maombolezo ya Sayyid al-Shuhadaa Imam Hussein (as) katika jiji la Arusha.
Tukio hilo, lililokamilika jioni ya jana, lilihudhuriwa na waumini wengi wa Ahlul-Bayt (as) pamoja na viongozi wa dini, ambapo bendera za Imam Hussein (as) zilipeperushwa kama ishara ya kuhuisha ujumbe wa Karbalaa na kuanza kwa siku za maombolezo ya mwezi wa Muharram.
Baada ya hafla hiyo, maeneo mbalimbali ya jiji la Arusha yalishuhudia kuanza kwa majlisi za kumbukumbu ya msiba wa Imam Hussein (as), huku waumini wakikusanyika katika misikiti, Husseiniya na vituo vya kidini kwa ajili ya kusikiliza mawaidha, darsa na historia ya tukio la Karbalaa.
Katika majlisi hizo, masheikh mbalimbali walipata fursa ya kuzungumza na waumini, wakieleza kwa kina mitihani mikubwa, mateso na changamoto alizokabiliana nazo Imam Hussein (as) katika safari yake ya kihistoria kuanzia Madina, Makka hadi ardhi ya Karbalaa, ambapo alisimama kidete katika kuitetea haki, uadilifu na maadili ya Uislamu wa kweli.
Waumini waliohudhuria majlisi hizo walisisitizwa kujifunza kutoka kwenye somo la Karbalaa, kuimarisha mshikamano wa Kiislamu na kuendeleza maadili ya kujitolea, subira na kusimamia haki katika jamii.
Maadhimisho ya Muharram katika jiji la Arusha yanatarajiwa kuendelea kwa siku kadhaa zijazo kwa ratiba mbalimbali za majlisi, mawaidha na shughuli za kidini zinazolenga kuhuisha ujumbe wa Imam Hussein (as).


na mashahidi wa Karbalaa.

Maoni yako