Jumamosi 25 Aprili 2026 - 21:33
Raddi amali ya Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qum kuhusu maneno ya kipuuzi ya rais mwenye dhana potofu wa Marekani

Hawza/ Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Kielimu ya Qum, kwa kuashiria umoja uliopo kati ya mihimili mitatu ya dola ya Iran, vikosi vya kijeshi na wananchi, imewataka watu wote kuwa macho mbele ya operesheni za kisaikolojia na vita vya propaganda vya adui vinavyolenga kupandikiza hofu na kudhuru umoja.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, maandishi ya ujumbe wa Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Kielimu ya Qum katika kujibu maneno ya kipuuzi ya rais mwenye dhana potofu wa Marekani—ambaye kwa lengo la kuleta mgawanyiko miongoni mwa viongozi wa nchi, aliwataja baadhi kuwa wakali na baadhi kuwa wa kati—ni kama ifuatavyo:

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu

Sifa iliyo wazi zaidi kwa siku hizi za Iran ni umoja na mshikamano wa kitaifa. Umoja huu umejengeka na unaonekana katika nguzo zote za mfumo wa Kiislamu kwa kuzunguka mhimili wa maelekezo ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu (baraka zake zidumu); kwa kushukuru neema hii ya umoja, tunainamisha paji la uso wetu kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu.

Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Kielimu ya Qum inapongeza umoja uliopo kati ya mihimili mitatu ya dola ya Iran, vikosi vya kijeshi na wananchi, na inawataka wote kuwa macho mbele ya operesheni za kisaikolojia na vita vya propaganda vya adui vinavyolenga kupandikiza hofu na kudhuru umoja ambao ni kipengele muhimu cha nguvu.

Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Kielimu ya Qum

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha