Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Dkt. Hayatu, mhadhiri wa masomo ya Kiislamu katika Chuo cha Shirikisho cha Dutsin-Ma (FUDMA), katika hafla rasmi ya uzinduzi wa chuo cha kwanza rasmi cha Qur’ani na usomaji wake mjini Katsina, alitoa wito wa kuongezwa juhudi za vijana na wanafunzi katika kuhifadhi Qur’ani Tukufu. Alibainisha kwamba; jambo hili linaongeza heshima na thamani ya nafsi kwa kila mwanadamu.
Aidha, Dkt. Gafidi Sani, mkurugenzi wa taasisi hiyo mpya, alisema kwamba; chuo hiki kimeanzishwa kwa ajili ya kuwafundisha wanafunzi katika taaluma za kuhifadhi Qur’ani Tukufu na usomaji wa kitaalamu kwa kutumia mbinu na njia zote mbalimbali zilizopo.
Chanzo: gazettengr.com
Maoni yako