Jumatatu 20 Aprili 2026 - 01:15
Simulizi ya kuvutia ya mwanachama wa msafara wa watu 72 kutoka Uturuki kuhusu Iran

Hawza/ Muhammad Shahid Karaz, mmoja wa wajumbe wa msafara wa “Marafiki wa Muqawama wa Uturuki” ambao wamesafiri kwenda Iran kwa ajili ya kuonesha mshikamano na nchi hiyo, katika maandishi yake alisisitiza juu ya nafasi ya msingi ya uwepo wa wananchi na kuendelea kwa shughuli za kila siku sambamba na mikusanyiko ya usiku.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, Muhammad Shahid Karaz, mmoja wa wajumbe wa msafara wa watu 72 wa “Marafiki wa Muqawama wa Uturuki” ambao wamekuja Iran katika mfumo wa msafara wa kiishara wa masahaba 72 wa Imam Hussein, katika ripoti ya uchunguzi wake wa moja kwa moja alielezea hali ya kijamii na mazingira ya jumla katika nchi hiyo.

Katika maandishi haya, huku akirejelea uwepo endelevu wa wananchi katika uwanja wa kijamii, alisema kuwa; jamii ya Iran sambamba na kuendelea kwa shughuli zake za kila siku, pia usiku hukusanyika katika viwanja na kuonesha uungaji mkono wake kwa muundo wa kisiasa na wa ulinzi wa nchi. Kwa mujibu wake, mwendelezo huu wa uwepo unaonesha kiwango cha juu cha mshikamano wa kijamii na ushiriki wa umma.

Karaz pia, akielezea mchakato huu kama “ustahimilivu endelevu”, alisisitiza kuwa kiwango hiki cha ushiriki wa wananchi kinapita mipaka ya mwenendo wa muda mfupi na kinaendelea kwa sura ya kudumu.

Simulizi ya kuvutia ya mwanachama wa msafara wa watu 72 kutoka Uturuki kuhusu Iran

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha