Jumanne 14 Aprili 2026 - 11:30

Hawza/ Mwenyekiti wa kamati ya kisheria ndani ya Hizbullah: Enyi ndugu wapiganaji wa jihadi na muqawama, enyi tegemeo la Umma na heshima na utukufu wake, Mwenyezi Mungu awaongezee malipo kwa sababu ya kuuwawa kishahidi kwa marji‘ wetu na kiongozi wetu, Imam Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la “Hawza”, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sheikh Muhammad Yazbek, mwenyekiti wa kamati ya kisheria Hizbullah na wakili wa kisheria wa Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei nchini Lebanon, alitoa ujumbe ambao ndani yake amesema: Enyi ndugu wapiganaji wa jihadi na muqawama, enyi tegemeo la Umma na heshima na utukufu wake, Mwenyezi Mungu awaongezee malipo kwa sababu ya shahada tukufu ya bwana wetu, heshima yetu na uhai wetu, marji‘ wetu na kiongozi wetu, Imam Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei. Ninyi ni neno jema na mti imara ambao mizizi yake iko ardhini na matawi yake yako mbinguni, unatoa matunda yake kila wakati na hautasimama katika nyakati zote mpaka ardhi iangazwe kwa nuru ya Mtukufu Mahdi (ajtf)

Aliongeza kuwa: Wao kwa jinai yao walitaka kuizima nuru ya Mwenyezi Mungu, lakini Mwenyezi Mungu hataki isipokuwa kukamilisha nuru Yake. Yeye kama babu yake Imam Hussein (as) yupo hai, na njia yake itaendelea pamoja nanyi na wapiganaji wote wa muqawama. Piganeni nao; Mwenyezi Mungu atawaadhibu kwa mikono yenu na atawaumbua na atawapa ushindi juu yao na ataponesha vifua vya watu waumini na ataondoa ghadhabu ya nyoyo zao.

Sheikh Yazbek aliendelea: Enyi mashujaa wa Hussein, kwa kupigana kwenu na kuwashambulia maadui wavamizi baada ya subira ndefu, huku damu zikichemka katika mishipa yenu, jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni msaidizi wenu; ameahidi kuwaadhibu maadui wenu na kuwafanya wanyonge kwa mikono ya roho safi ambazo hubadilisha mizani na kutekeleza ushindi kwa ahadi ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu kupitia kwenu ataponya vifua vya Waumini na ataondoa ghadhabu ya nyoyo zao, na Yeye ndiye aliyesema: «وَمَا رَمَیْتَ إِذْ رَمَیْتَ وَلَکِنَّ اللَّهَ رَمَی». Ninyi ni wana wa Imam Ali (as); mnafanya kwa mujibu wa kauli yake aliposema: “Ufanisi ni kwa yule anayeingia katika hatari, na maangamizi ni kwa yule anayesitasita.” Yule anayesitasita huwa na shaka na hubaki bila upande, na kutokuegemea upande wowote hakuleti chochote isipokuwa udhalili na aibu zaidi.

Mjumbe mwandamizi wa Hizbullah alisema: Je, wanaolingana kwenye kutokuegemea upande wowote hawajui kwamba wakimuacha adui, adui hatawaacha, bali hatawaacha mpaka ahakikishe matakwa yake juu yao kwa udhalilifu na utumwa? Ninyi, enyi wema, baada ya Mwenyezi Mungu, nnyinyi ndio matumaini; mnatengeneza mazingira kwa ajili ya Imam anayengojewa, Mahdi (ajtf). Mmeitikia wito wa Mwenyezi Mungu na Mtume Mtukufu (saww) na hamkuogopa vitisho vya kutisha. Ninyi ndio wale ambao Mwenyezi Mungu amesema kuhusu wao:


«الَّذِینَ قَالَ لَهُمُ النَّاسُ إِنَّ النَّاسَ قَدْ جَمَعُوا لَکُمْ فَاخْشَوْهُمْ فَزَادَهُمْ إِیمَانًا وَقَالُوا حَسْبُنَا اللَّهُ وَنِعْمَ الْوَکِیلُ * فَانقَلَبُوا بِنِعْمَةٍ مِّنَ اللَّهِ وَفَضْلٍ لَّمْ یَمْسَسْهُمْ سُوءٌ وَاتَّبَعُوا رِضْوَانَ اللَّهِ وَاللَّهُ ذُو فَضْلٍ عَظِیمٍ».

Ninyi ni kama alivyonena Amirul-Mu’minin (as): “Ninyi ni wasaidizi wa haki, ndugu wa dini, na ngao ya siku ya shida; hakuna kitu kinachowatuliza isipokuwa haki, wala hakuna kitu kinachowakimbiza isipokuwa batili.” Na ni kwa mikono yenu safi ndipo ushindi, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, utapatikana.

Sheikh Yazbek katika hitimisho alisema: Enyi watu wetu watukufu, enyi watu wa muqawama na wanaouunga mkono, enyi wapendwa waheshimiwa; kama ambavyo watoto wenu na vipenzi vyenu ni simba wa mapambano na wapanda farasi wa medani, na kama wao hawana mfano, ninyi pia ni watu wa uchamungu na fadhila; wenye nguvu katika dini, wenye imani thabiti, wavumilivu katika matatizo na mlioshikamana na haki.

Ikiwa kutengana na nyumba na kuwa mbali na wapendwa wenu kunawatisha, basi kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kumkimbilia Yeye kutawapa utulivu; na mna yakini kwamba utatuzi wa mambo upo mikononi mwa Mwenyezi Mungu na kila kitu kinaendelea kwa qadari Yake. Enyi wapendwa, yale mnayopitia yanaielemea mioyo yetu; Mwenyezi Mungu awapokee na awalipe kwa subira na uthabiti wenu. Ninyi ni familia za mashahidi, majeruhi na mateka, na sisi hatutawaacha kamwe mateka wetu, kama ilivyokuwa wosia wa shahidi mkubwa wa Umma, Sayyid Hassan Nasrallah (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake), aliyesema: Sisi ni watu ambao hatuwaachi mateka wetu magerezani. Kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu, wapiganaji watafanikiwa kuwaokoa, na dua yetu kwa majeruhi ni kwamba; Mwenyezi Mungu awape shifaa na afya njema. Muishi daima enyi watu wetu; hifadhi na utayarishaji wa mazingira ni kwa ajili ya Imam Mahdi (ajtf).


إنهم یرونه بعیداً ونراه قریباً، وما النصر إلا صبر ساعة وإنه آت آت بإذن الله تعالی والسلام علیکم ورحمة الله وبرکاته.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha