Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama chaShirika la Habari la Hawza, Mkusanyiko wa Wanazuoni wa Jabal ‘Amil, kupitia tamko rasmi kufuatia shahada ya Sheikh Sadiq al-Nabulsi, ulisema: Kwa ridhaa kamili juu ya qadhaa ya Mwenyezi Mungu na kwa nyoyo zilizojaa huzuni na hasira, tunatoa pole kwa taifa pendwa la Lebanon, kwa Umma wa Kiislamu, na kwa watu wote huru duniani, kwa shahada ya Sheikh Sadiq al-Nabulsi.
Matini ya tamko hilo ni kama ifuatavyo:
Kwa ridhaa kamili juu ya qadhaa ya Mwenyezi Mungu na kwa nyoyo zilizojaa huzuni na hasira, tunatoa pole kwa taifa pendwa la Lebanon, kwa Umma wa Kiislamu na kwa watu wote huru duniani, kwa shahada ya Sheikh Sadiq al-Nabulsi; yeye ambaye tarehe 8 Aprili 2026, akiwa na umri wa miaka hamsini na moja, alipata shahada kutokana na shambulizi la anga la Kizayuni lililolenga majengo ya “al-Sayyida al-Zahraa” katika mji wa Saida. Majengo haya ya kidini yalikuwa yakijumuisha msikiti, Husseia na “Hawza ya Imamu Sadiq (as)” kwa ajili ya elimu za dini, ambayo yeye alikuwa msimamizi na mwalimu wake. Katika shambulizi hilo, yeye pamoja na idadi kubwa ya wafanyakazi na waliokimbia makazi yao, walipata shahada.
Shahidi al-Nabulsi ni mwana wa marehemu Ayatullah Sheikh Afif al-Nabulsi; miongoni mwa shakhsia mashuhuri za Hawza ya kielimu huko Jabal ‘Amil na mmoja wa watu muhimu katika njia ya muqawama wa Kiislamu kusini mwa Lebanon. Pia ni ndugu wa Shahidi Hajj Muhammad Afif al-Nabulsi na mjomba wa Shahidi Muhammad Baqir al-Nabulsi; katika familia ambayo imetoa sadaka kubwa, ambamo elimu imeunganishwa na jihadi na neno na vitendo vimechanganyika.
Shahidi al-Nabulsi alikuwa sauti ya kielimu na kifikra katika uwanja wa kutetea haki na mimbari yenye uelewa katika kukabiliana na uvamizi na dhulma; aliunganisha kati ya neno la kweli na msimamo thabiti, hadi Mwenyezi Mungu akahitimisha maisha yake kwa shahada; katika njia ambayo daima aliihimiza na kuiamini.
Sisi huku tukimuaga mwanachuoni huyu mujahid, tunalaani na kukemea kwa maneno makali zaidi mauaji ya kutisha ya Kizayuni; mauaji ambayo yalijumuisha zaidi ya mashambulizi 134 ya anga na kusababisha zaidi ya mashahidi na majeruhi elfu moja; mashambulizi ya makusudi na ya kinyama yaliyolenga mikusanyiko ya waliokimbia makazi yao, bila kuheshimu hata kidogo utu wa binadamu au utakatifu wa maeneo. Uvamizi huu pia ulihusisha vituo vya ibada na maeneo ya kidini, jambo ambalo ni uvunjaji wa wazi wa maadili yote ya kimungu na mikataba ya kimataifa.
Shambulizi hili la kinyama, pamoja na madhara yake hatari, kwa mara nyingine linathibitisha asili ya uhalifu ya utawala wa Kizayuni na kutokujali kwake mila na sheria zote, na ni doa jingine la aibu katika paji la uso wa ukimya wa kimataifa na udhaifu wa Kiarabu na Kiislamu, ambao kwa ukimya na uzembe wao wamekuwa washirika katika uhalifu huu.
Kwa msingi huo, tunamchukulia adui Muisraeli kuwa ndiye mwenye jukumu kamili la mauaji haya na madhara yake hatari, na tunasisitiza kushikamana na chaguo la muqawama; chaguo ambalo ni haki halali ya kukabiliana na uvamizi na uchokozi na ni dhamana ya kulinda ardhi, watu na mamlaka. Tunaona kuongezeka kwa uhalifu wa adui kuwa ni sababu inayolazimisha kuongeza uthabiti katika majibu na kuinua kiwango cha mapambano ili kudhibiti uvamizi na kuuzuia kuendelea.
Pia tunaiita serikali ya Lebanon ibebe majukumu yake ya kitaifa katika kuwasaidia wananchi, kuwahudumia majeruhi na familia za mashahidi, na kulinda heshima ya taifa. Aidha, tunaziomba taasisi za kimataifa na za kibinadamu zichukue hatua za haraka kusitisha uhalifu huu na kuwafikisha wahusika mbele ya sheria.
Na tunawaomba watu huru duniani wasimame kwa sauti kubwa dhidi ya dhulma hii na wawaunge mkono wanyonge kwa njia zote halali.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu amrehemu kwa rehema zake pana Shahidi Sheikh Sadiq al-Nabulsi, amjumuishe pamoja na Manabii, wasema kweli, Mashahidi na watu wema, awape majeruhi uponyaji wa haraka na azijalie familia za mashahidi subira na utulivu.

Maoni yako